Ticker

6/recent/ticker-posts

DIWANI KATA YA LUCHELELE AIPONGEZA TARURA

Diwani wa Kata ya Luchelele Vicent Tegge akizungumza na Mwandishi wa habari wa Sayari news juu ya utekelezaji wa miradi kwenye kata hiyo.

***********************

Na Sheila Katikula,Mwanza

Diwani wa Kata Luchelele Vincent Tege ameipongeza Wakala wa barabara wa vijijini na mjini (TARURA) kwa kufanikiwa kujenga barabara kiwango cha lami urefu wa kilometa 1.5 kwenye kata hiyo.

Amesema ujenzi huo imefanyika kutoka chuo kikuu cha mtakatifu Agustino (SAUT) kwenda Luchelele umekamilika na kupelekea wananchi kupata usafiri wa uhakika sehemu hiyo.

Pongezi hizo zimetolewa na diwani hivi karibuni jijini Mwanza alipokuwa anazungumza na Sayari news ofisini kwake.

Amesema ujenzi wa barabara hiyo umekamilika kutokana na fedha zilizotolewa kutoka serikalini na kwa sasa eneo hilo limeelekeza juhudi kubwa katika ujenzi wa vyumba vya sekondari.

Amesema wanatarajia kujenga shule Mpya ya Sekondari eneo la Shadi lilotengwa na serikali mwaka 2006/7 na lilikuwa halijalipiwa fidia kwa wakaazi wa sehemu hiyo.

Diwani huyo ameipongeza Halmashauri ya Jiji la Mwanza kwa kutenga zaidi ya sh milioni 49 kulipa fidia kwa wananchi wa eneo hilo lilotengwa Kwa ajilinya ujenzi wa shule.

"Tunategemea kuanza kulipa fidia kwa wananchi na tuanze ujenzi wa shule hiyo nawaomba wananchi waendelee kutoa ushirikiano katika miradi inayotekelezwa,"amesema Tegge.

"Wananchi katika eneo hilo wameanza kuchanga michango na mimi nimechangia tripu 20 za mawe ili tuweze kuanza ujenzi huu,"amesema Tegge

Post a Comment

0 Comments