Ticker

6/recent/ticker-posts

DC MBONEKO AZINDUA VITABU VYA KUBORESHA ELIMU MANISPAA YA SHINYANGA, AONYA WAZAZI KUDHALILISHA WALIMU

 


Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akionesha Vitabu vya Mkakati wa Kuboresha Elimu nchini leo Ijumaa Septemba 16,2022 kwenye kikao cha wadau wa elimu katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Getrude Gisema.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akionesha Vitabu vya Mkakati wa Kuboresha Elimu nchini leo Ijumaa Septemba 16,2022 kwenye kikao cha wadau wa elimu katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.Kulia ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhani Masumbuko, kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Getrude Gisema.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko amezindua Vitabu vya Mkakati wa Kuboresha Elimu nchini katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga huku akihamasisha nidhamu shuleni na kupiga vita vitendo vya baadhi ya wazazi kudhalilisha walimu, utoro, ndoa na mimba za utotoni.

Uzinduzi huo umefanyika leo Ijumaa Septemba 16,2022 wakati wa kikao cha wadau wa elimu Manispaa ya Shinyanga kilichofanyika katika ukumbi wa shule ya Msingi Buhangija Manispaa ya Shinyanga.


Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, ulioenda sanjari na kugawa vitabu kwa maafisa elimu kata, wakuu wa shule na walimu wakuu, Mboneko amesema vitabu hivyo vitatumika kuboresha elimu huku akionya vitendo vya udhalilishaji vinavyofanywa na baadhi ya watu wakiwemo wazazi ambao wamekuwa wakidiriki kutukana na kuwafanyia udhalilishaji.

“Tunataka nidhamu iendelee kuwepo shuleni, walimu mfanye kazi kwa amani na mnaheshimika. Lazima mjiheshimu na mtu yeyote ambaye hawezi kumheshimu mwalimu na kufikia hatua ya kumfanyia udhalilishaji lazima tumshughulikie, lazima tumsaidie matatizo yake. Kwanini utukane au kupiga mwalimu?, umdhalilishe?”,amesema Mboneko.

“Sitaki kusikia kuna utoro wala kuona Sifuri kwenye shule za wilaya ya Shinyanga, tunachotaka kuona ni shule zote Shinyanga zinakuwa na ufaulu mzuri. Nataka kuona watoto wanafundishwa na kufaulu kwenye mitihani yao. Ili kuwa na matokeo mazuri ni jukumu la mzazi na mwalimu na jamii kwa ujumla kushirikiana”,ameongeza mkuu huyo wa wilaya.

Amesema serikali inaendelea kuboresha miundombinu shuleni huku akiwaomba walimu kufanya kazi kwa weledi na kuzingatia maadili ya kazi yao.

“Kila shule inapata vitabu hivi ambavyo vimetumia gharama kubwa. Msiende kuvihifadhi tu bali nendeni mkavisome,mvielewe na kutekeleza maelezo yanayotolewa na serikali ili kuboresha elimu nchini. Vitabu hivi vikafanye kazi kweli kweli na mvitumie kwa ufanisi mkubwa”,amesema Mboneko.

Kwa upande wake, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhani Masumbuko amewataka walimu kuvaa vizuri na kuepuka ulevi.

“Tuwe na tabia nzuri ili kuboresha elimu, Walimu wavae vizuri, ulevi, kuna walimu wanalewa pombe. Kama mwalimu hujiheshimu ni vigumu wanafunzi kukuheshimu. Hata lugha zetu ziwe nzuri mfano mwalimu unasema ‘Jero’. Mwalimu ni lazima uwe tofauti. Lakini pia Viongozi wa juu kudhalilisha walimu siyo ustarabu, unakuta kiongozi flani anakagua shule lakini anamfokea mwalimu”,amesema Masumbuko.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Getrude Gisema amesema halmashauri imejipanga vizuri kuhakikisha inaboresha sekta ya elimu na kuendelea kufanya vizuri kwenye mitihani.

Kwa upande wake, Afisa Elimu Sekondari Manispaa ya Shinyanga, Lucas Mzungu amevitaja Vitabu hivyo ni pamoja na  kitabu cha Mkakati wa Kuimarishaji Ufundishaji na Ujifunzaji Ngazi ya Elimu MsingiKitabu cha Changamoto katika Uboreshaji wa Elimu Msingi na Sekondari. Nini Kifanyike? pamoja na Kitabu cha Mwongozo wa Uteuzi wa Viongozi wa Elimu katika Mamlaka za Serikali za Mitaa na Mikoa.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza kwenye kikao cha wadau wa elimu katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa ajili ya kuzindua Vitabu vya Mkakati wa Kuboresha Elimu nchini kilichofanyika leo Ijumaa Septemba 16,2022 katika ukumbi wa shule ya msingi Buhangija Mjini Shinyanga. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza kwenye kikao cha wadau wa elimu katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa ajili ya kuzindua Vitabu vya Mkakati wa Kuboresha Elimu nchini
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Getrude Gisema akizungumza kwenye kikao cha wadau wa elimu katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa ajili ya kuzindua Vitabu vya Mkakati wa Kuboresha Elimu nchini.
Afisa Elimu Sekondari Manispaa ya Shinyanga, Lucas Mzungu akizungumza kwenye kikao cha wadau wa elimu katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa ajili ya kuzindua Vitabu vya Mkakati wa Kuboresha Elimu nchini.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhani Masumbuko akizungumza kwenye kikao cha wadau wa elimu katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa ajili ya kuzindua Vitabu vya Mkakati wa Kuboresha Elimu nchini.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizindua Vitabu vya Mkakati wa Kuboresha Elimu nchini leo Ijumaa Septemba 16,2022 kwenye kikao cha wadau wa elimu katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga. Kulia ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhani Masumbuko, kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Getrude Gisema.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (kushoto) akigawa Vitabu vya Mkakati wa Kuboresha Elimu nchini. Vitabu hivyo vimegawiwa kwa maafisa elimu kata, wakuu wa shule na walimu wakuu katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (kushoto) akigawa Vitabu vya Mkakati wa Kuboresha Elimu nchini. Vitabu hivyo vimegawiwa kwa maafisa elimu kata, wakuu wa shule na walimu wakuu katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (kushoto) akigawa Vitabu vya Mkakati wa Kuboresha Elimu nchini. Vitabu hivyo vimegawiwa kwa maafisa elimu kata, wakuu wa shule na walimu wakuu katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (kushoto) akigawa Vitabu vya Mkakati wa Kuboresha Elimu nchini. Vitabu hivyo vimegawiwa kwa maafisa elimu kata, wakuu wa shule na walimu wakuu katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
Wadau wakiwa kwenye kikao cha wadau wa elimu Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa ajili ya kuzindua Vitabu vya Mkakati wa Kuboresha Elimu nchini
Wadau wakiwa kwenye kikao cha wadau wa elimu Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa ajili ya kuzindua Vitabu vya Mkakati wa Kuboresha Elimu nchini
Wadau wa elimu wakiwa kwenye kikao cha uzinduzi wa Vitabu vya Mkakati wa Kuboresha Elimu nchini
Wadau wa elimu wakiwa kwenye kikao cha uzinduzi wa Vitabu vya Mkakati wa Kuboresha Elimu nchini.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog



Post a Comment

0 Comments