RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Mwinyi akihutubia katika chakula maalum cha mchana na kuwapongeza na kuwazawadia zawadi Wanafunzi wa Kidatu cha Nne na cha Sita Unguja waliofanya vizuri Mitihani yao ya Taifa na kufaulu vizuri, hafla hiyo iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar leo 3-8-2022.(Picha na Ikulu)
WANAFUNZI wa Kidatu cha Sita na Nne Skuli za Sekondari Unguja wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) wakati wa hafla ya Chakula maalum cha mchana na kuzawadia zawadi kwa kufaulu vizuri mitihani yao ya Taifa, hafla hiyo iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar leo 3-8-2022.(Picha na Ikulu) RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimkabidhi zawadi ya Lapto Mwanafunzi Nasra Ali Omar wa Skuli ya Zanzibar Commercial na ametokea Mwanafunzi 10 Bora Kitaifa Wanawake kwa Tahasusi ya ECA, na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Lela Mohammed Mussa, hafla hiyo iliyofanyika leo 3-8-2022 katika viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu) MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akimkabidhi zawadi ya Fedha Mwanafunzi Bora nafasi kumi Kitaifa Wanawake Tanzania wa Skuli ya Zanzibar Commercial Kidatu cha Sita Nasra Ali Omar, wakati wa hafla ya Chakula Maalum na kuzawadiwa zawadi na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, Wanafunzi Bora waliofanya vizuri Mitihani yao ya Taifa, katika viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakiwa katika picha ya pamoja na Wanafunzi Bora wa Kidatu cha Sita (kulia kwa Mama Mariam Mwinyi) Mwanafunzi Nasra Ali Omar (Skuli ya Zanzibar Commercial) Mwanafunzi Marco Andra Masabula (Lumumba) na (kushoto kwa Rais) Idrisa Ali Shaban (Skuli ya Zanzibar Commercial) Nahya Said Ahmed (Skuli ya Zanzibar Commercial ) na Firdaaus Salum Seif (FEZA) (Picha na Ikulu)
0 Comments