Ticker

6/recent/ticker-posts

MRADI WA TGNP KUHAMASISHA WANANCHI KUSHIRIKI HARAKATI ZA MAENDELEO WALETA MANUFAA HALMASHAURI YA MOROGORO

 

MRADI wa kuhamasisha wananchi kushiriki harakati za maendeleo unaotekelezwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) katika Kata tatu za Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro umeleta manufaa kwa wananchi wilayani humo.


Mradi huo ambao pia unalenga wananchi kujitambua, kushiriki na kuhoji matumizi ya fedha za rasilimali za nchi unatekelezwa katika Kata tatu za Kisaki, Bwakira chini na Mngazi.


Asma Kilonga ambaye ni mjasiriamali na Katibu wa Kituo cha Taarifa na Maarifa (KC) Kata ya Kisaki ni mmoja wa wanufaika wa mradi huo ambaye amefanikiwa kupiga hatua kimaendeleo kupitia mradi huo.


Asma anasema baada ya kupata mafunzo ya mradi kutoka TGNP kupitia Kituo cha Taarifa na Maarifa aliamua kulima shamba lake mwenyewe la viazi lishe japo alipambana katika kutafuta soko lakini kwa sasa amefanikiwa na biashara yake inakwenda vizuri.


“Mimi nilithubutu kulima shamba langu mwenyewe la viazi baada ya kupata mafunzo na kupenda mradi huu wa viazi. Kwa sababu nilikuwa nalinganisha nikilima heka moja ya viazi na ufuta tayari nikaona tofauti. Kwa hiyo nikachukua mbegu nikapanda heka moja na nusu. Katika hiyo heka moja na nusu, heka moja nikawahi kupanda, hiyo nusu nikachelewa kidogo lengo ni kuangalia bei kama itakuwa na uwiano sawa. Ile heka moja niliyoipanda nikaenda nayo ilivyofika mwezi wa sita nikaangalia viazi nikavikuta viko tayari.” Anasema Asma.



Asma anasema alipitia changamoto nyingi katika kuhakikisha anapata soko la viazi vyake na baada ya kupambana mwenyewe bila kukata tamaa hatimaye alipata soko na kuuza viazi vyake.


Si hivyo tu, lakini mwanamama huyu pia alithubutu kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ikiwemo udiwani ambao hata hivyo anasema kura hazikutimia na kwamba wakati ujao anaamini zitatimia na kushika wadhifa huo.


“Elimu niliyoipata TGNP, hapa nilipo kwanza ni Mjumbe wa Hlamashauri ya Kijiji niligombea, na pia nilithubutu kuchukua fomu ya udiwani wa Kata kwa bahati mbaya kura zangu hazikutosha. Kwa hiyo sasa nina uwezo wa kusimama kwenye mkutano wa Kijiji kuelimisha wat una siogopi mtu wa aina yeyote, nasimama na kuwea kuzungumza na mtu wa aina yeyote. TGNP wamenipa uraghibishi wamenijengea uwezo nawashukuru sana.” Anasema Asma.



Naye Rukia Jambalaga ambaye ni mfugaji wa kuku kupitia Kituo cha Taarifa na Maarifa Kata ya Bwakira Chini anasema baada ya kupata elimu ya ufugaji wa kuku kutoka Ushirika wa Wajasiriamali Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sua (SUGECO) kupitia TGNP amepata maendeleo makubwa baada ya kuanza ufugaji na kuuza kuku ambapo alifanikiwa kujenga nyumba ya kisasa.


“Kwanza tunashukuru kupata mafunzo haya ya TGNP, yametukwamua sana kimaisha. Kwanza elimu tumeenda kupata Sugeco ya mafunzo ya kufuga kuku. Kwa kweli tulipotoka na sugeco mpaka kufika hapa mafanikio tuliyoyapata ni makubwa sana kiasi ambacho tangu nilipoingia kwenye KC hii mpaka sasa hivi nina maendeleo makubwa. Tumeanza mradi wa kufuga kuku, tumeenda kuchukua kuku elfu moja tukaja tukafuga, kuku wale wakawa wakubwa na tumewauza tumepata zaidi ya mamilioni.” Anasema Rukia.


Rukia anasema kuwa baada ya kupata fedha hizo waliamua kwenda kuchukua kuku wengine ili mradi wao uendelee na kuamua kwa kila mwanakikundi kujifunza nyumbani kwake namna ya ufugaji bora ili kila kila mmoja aweze kufuga.


Anasema alianza kwa kufuga kuku mia tano na baada ya biashara kumwendea vizuri aliweza kujenga nyumba ya kisasa ya vyumba sit ana hivyo kuishukuru TGNP kwa kuwapelekea mradi huo.


Mradi wa Kituo cha Taarifa na Maarifa (KC) kupitia mpango wa uraghibishi umewasaidia kwa kiasi kikubwa wananchi wa maeneo hayo kufahamu mambo mengi ambayo hapo awali hawakuwa wakiyafahamu.


Miongoni mwa mambo hayo ni pamoja na haki ya umiliki wa ardhi kwa wanawake, changamoto katika sekta ya elimu, uongozi na afya ambapo baada ya kupatiwa mafunzo ya uraghibishi wananchi walipata mwamko katika kupigania kuondoa changamoto hizo.


Severine Henry Msohela ambaye ni mmoja wa wanachama wa kikundi cha taarifa na maarifa (KC) Kata ya Kisaki anasema baada ya TGNP kuwapatia mafunzo hayo mwaka 2013, mambo mengi yamebadilika baada ya wananchi kujengewa uwezo
Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Lilian Liundi (kulia) akisalimiana na wanamtandao wa Kikundi cha Taarifa na Maarifa (KC) Kata ya Bwakira Chini, Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro, wakati yeye na maofisa wengine wa mtandao huo walipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya miradi ya mtandao huo katika Kata za Bwakira Chini, Mngazi na Kisaki hivi karibuni.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Lilian Liundi akizungumza na wanamtandao wa Kikundi cha Taarifa na Maarifa (KC) Kata ya Bwakira Chini, Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro, wakati yeye na maofisa wengine wa mtandao huo walipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya miradi ya mtandao huo katika Kata za Bwakira Chini, Mngazi na Kisaki hivi karibuni.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Lilian Liundi akiwa kwenye majadiliano na wanamtandao wa Kikundi cha Taarifa na Maarifa (KC) Kata ya Bwakira Chini, Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro, wakati yeye na maofisa wengine wa mtandao huo walipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya miradi ya mtandao huo katika Kata za Bwakira Chini, Mngazi na Kisaki hivi karibuni.
Meneja wa Fedha wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Altho Mwangoa akiwa kwenye majadiliano wanamtandao wa kikundi cha Taarifa na Maarifa Kata ya Bwakira Chini, Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro, wakati yeye na maofisa wengine wa mtandao huo walipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya miradi ya mtandao huo katika Kata za Bwakira Chini, Mngazi na Kisaki hivi karibuni.
Wanamtandao wa kikundi cha Taarifa na Maarifa Kata ya Mngazi, Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa na wawezeshaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) walipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya miradi ya mtandao huo katika Kata za Bwakira Chini, Mngazi na Kisaki hivi karibuni.
Wanamtandao wa kikundi cha Taarifa na Maarifa Kata ya Mngazi, Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro wakiwa kwenye majadiliano na viongozi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kuhusu maendeleo ya mradi wao wakati watendaji wa mtandao huo walipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya miradi ya mtandao huo katika Kata za Bwakira Chini, Mngazi na Kisaki hivi karibuni.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Lilian Liundi akiwa kwenye majadiliano na wanamtandao wa Kikundi cha Taarifa na Maarifa (KC) Kata ya Kisaki, Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro, wakati yeye na maofisa wengine wa mtandao huo walipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya miradi ya mtandao huo katika Kata za Bwakira Chini, Mngazi na Kisaki hivi karibuni.

Wanamtandao wa kikundi cha Taarifa na Maarifa Kata ya Kisaki, Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa na wawezeshaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) walipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya miradi ya mtandao huo katika Kata za Bwakira Chini, Mngazi na Kisaki hivi karibuni.

Post a Comment

0 Comments