Ticker

6/recent/ticker-posts

KATIBU MKUU KIONGOZI BALOZI KATTANGA ATEMBELEA BANDA LA TVLA KWENYE MAONESHO NANENANE MBEYA


Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi Hussein A. Kattanga akipata maelezo kutoka kwa Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Bw. Tixon Nzunda kuhusiana na Wizara ilivyojipanga kupunguza vifo vya Mifugo kwa kutumia chanjo zinazozalishwa na Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) kwa kufuata ratiba ya kitaifa ya uchanjaji wa Mifugo inayoratibiwa na Wizara siku ya tarehe 07/08/2022 alipotembelea banda la Wakala kwenye Maonesho ya Nanenane yanayofanyika kitaifa Jijini Mbeya kwenye viwanja vya John Mwakangale.

Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi Hussein A. Kattanga akipata ufafanuzi kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania Dkt. Stella Bitanyi kuhusiana na Wakala inavyohakiki ubora wa vyakula vya mifugo siku ya tarehe 07/08/2022 alipotembelea banda la Wakala lililopo ndani ya banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye Maonesho ya Nanenane yanayofanyika kitaifa Jijini Mbeya kwenye viwanja vya John Mwakangale.

Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania Dkt. Stella Bitanyi akitoa ufafanuzi kwa Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi Hussein A. Kattanga kuhusiana na aina saba za Chanjo zinazozalishwa na Wakala siku ya tarehe 07/08/2022 alipotembelea banda la Wakala lililopo ndani ya banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye Maonesho ya Nanenane yanayofanyika kitaifa Jijini Mbeya kwenye viwanja vya John Mwakangale. Aliesimama nyuma yake ni Kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Bw. Tixon Nzunda.

Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi Hussein A. Kattanga akisaini kitabu cha wageni alipotembelea kwenye Banda la Wakala wa Maabara ya Veterinari Tanzani (TVLA) lililopo ndani ya banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi alipotembelea kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na wakala siku ya tarehe 07/08/2022 kwenye Maonesho ya Nanenane yanayofanyika kitaifa Jijini Mbeya kwenye viwanja vya John Mwakangale. Waliosimama nyuma yake kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Bw. Tixon Nzunda, kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Dkt. Rashid Tamatamah na aliesimama mbele yake ni. Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania Dkt. Stella Bitanyi.

Post a Comment

0 Comments