Meneja wa Benki ya Exim Tawi la Mbeya Bw Peter Mwamala (wa pili kulia) akizungumza na wadau wa kilimo waliotembelea banda la maonesho ya kilimo la benki hiyo inayoshiriki Maonesho ya Kilimo Nanenane yanayofanyika katika Uwanja wa John Mwakangale mkoani Mbeya.
Mmoja wa maofisa wa Benki ya Exim tawi la Mbeya Bi Hidelita Mwapinga (kushoto) akizungumza na wadau wa kilimo waliotembelea banda la maonesho ya kilimo la benki hiyo inayoshiriki Maonesho ya Kilimo Nanenane yanayofanyika katika Uwanja wa John Mwakangale mkoani Mbeya.
Tupo tayari kuwahudumia! Timu ya maofisa wa benki ya Exim tawi la Mbeya wakiongozwa na Meneja wa Benki hiyo Tawi la Mbeya Bw Peter Mwamala (wa tatu kulia) wakiwa kwenye picha ya pamoja kwenye banda la maonesho ya kilimo la benki hiyo inayoshiriki Maonesho ya Kilimo Nanenane yanayofanyika katika Uwanja wa John Mwakangale mkoani Mbeya.
..........................................
Huduma zinazotolewa na Benki ya Exim Tanzania kwa wadau wa sekta ya kilimo zimeendelea kuwavutia washiriki wengi wa Maonesho ya Kilimo Nanenane yanayofanyika katika Uwanja wa John Mwakangale mkoani Mbeya.
Kwa mujibu wa Meneja wa Benki hiyo Tawi la Mbeya Bw Peter Mwamala, alisema taasisi hiyo imejipanga kuhakikisha inayatumia vema maonesho haya kutambulisha zake kwa wadau mbalimbali wa sekta ya kilimo nchini wakiwemo wakulima, wachakataji wa bidhaa za mazao pamoja na wasambazaji.
“Tunashiriki maonesho haya tukiwa na dhamira kuu ya kuwa karibu zaidi na wakulima kwa kuhakikisha kwamba wanazifahamu huduma zetu zinazohusiana na sekta ya kilimo ikiwemo huduma za malipo pamoja na fursa za mikopo. Zaidi pia tunayatumia maonesho haya kupata kutoa huduma zetu za kifedha kwa wateja wetu waliopo kwenye maonesho haya huku pia tukipata mrejesho wa huduma zetu kutoka kwa wateja,’’ alisema.
0 Comments