Mkuu wa Wilaya ya Mafia Mandisi Martin Ntemo akikagua mbegu za miti alipotembelea Banda la wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) kwenye maonesho ya nanenane kanda ya Mashariki yanayoendelea Mkoani Morogoro.
Mkuu wa Wilaya ya Mafia Mandisi Martin Ntemo akisikiliza maelezo ya namna ya kufuga na kuvuna asali ya nyuki wadogo alipotembelea Banda la wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) kwenye maonesho ya nanenane kanda ya Mashariki Mkoani Morogoro.
Mkuu wa Wilaya ya Mafia Mandisi Martin Ntemo akikagua miche ya miti mbalimbali kwenye Banda la wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) kwenye maonesho ya nanenane kanda ya Mashariki Mkoani Morogoro.
*******************************
NA FARIDA SAID, MOROGORO.
Halmashauri za mikoa ya Pwani,Tanga Dar es Salaam na Morogoro zinazounda kanda ya mashariki ya maonesho ya Nanenane wametakiwa kushirikiana na WAKALA wa huduma za misitu nchini TFS katika kuzalisha miche ya miti ili kuweza kufikia lengo la kupanda miti milioni moja na nusu kwa mwaka
Hayo yamebainshwa na Mkuu wa Wilaya ya Mafia Mandisi Martin Ntemo wakati alipotembelea Banda la TFS katika maonyesho hayo yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Mkoani Morogogoro
Mhandisi Ntemo alisema kuwa ni vyema jamii ikapanada miti katika mipaka ya maeneo yao ili kuepuka migogoro ya ardhi inayoendelea kwenye baadhi ya maeneo hapa nchini.
“Tunaweza kutumia miti kama sehemu ya kuonesha mipaka katika maeneo yetu, hii itasaidia sana kupunguza hii migogoro ya ardhi inayotokana na mipaka inayoendelea kwenye baadhi ya maeneo.” Alisema Mhandisi Ntemo.
Pia amewaomba wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) kuendelea kuhamasisha upandaji wa miti katika maeneo mbalimbali ya nchi na uhifadhi wa mazingira kwa kutunza vyanzo vya maji ilikuepukana na mabadiliko ya tabia nchi yaliyo sababishwa na shughuli za kibina damu.
Aidha Mandisi Ntemo ameishauri TFS kushirikina na vyema na wakandarasi wanaotekeleza miradi mbalimbali hapa nchini katika utunzaji wa mazingira hasa panapotokea uharibifu wa misitu ili iweze kurejeshwa katika hali yake ya awali.
Kwa upande wake Meneja msaidizi wa TFS upande wa Rasilima za msitu Kanda ya Mashariki Michael Ntilicha amesema kuwa wameendelea kutoa elimu katika maonyesho hayo ikiwemo kutumia samani zinazotokana na mianzi.
Alisema pamoja na kutoa elimu Mamlaka hiyo pia imeendelea kupanda miti katika mashamba yao na kuzalisha miche ya miti ambayo hutolewa kwa wananchi lengo likiwa ni kuendelea kutunza mazingira.
Nao wananchi waliotembelea Banda la TFS wamesema wamepata elimu juu ya utunzaji wa mazingira pamoja na umuhimu wa kupanda miti katika maeneo yao,ambapo wameahidi kwenda kwenda kupanda miti ili kufikia lengo la serikali la kupanda miti milioni moja kwa mwaka kwa kila Halmashauri.
0 Comments