Waimbaji wa Kwaya ya Gethsemane Group Kinondoni SDA wakiwa pamoja baada ya kuzindua rasmi video ya wimbo mpya unaofahamika kwa jina la Nitengeneze Upya Bwana.
****************
Na Mwandishi Wetu
KWAYA maarufu nchini ya Gethsemane Group Kinondoni SDA imetoa video ya wimbo wake mpya unaoitwa Nitengeneze Upya Bwana ikiwa ni muendelezo wa kwaya hiyo kutoa nyimbo za kumsifu na kumuabudu Bwana.
Taarifa iliyotolewa na uongozi wa kwaya ya Gethsemane Group Kinondoni jijini Dar es Salaam umesema wimbo kwa sasa umeshazinduliwa na unapatikana kwenye mitandao yao ya kijamii.
"Tumetoa wimbo mpya unaoitwa Nitengeneze Upya Bwana na tayari unapatikana youtube kwenye channel yetu. Kupata channel, ingia youtube na kuandika Gethsemane Group Kinondoni SDA na wataona wimbo lakini pia utakua unapigwa kwenye vyombo vya Habari vyote
"Tunafahamu wapo ndugu zetu ambao watataka kufahamu Wimbo wetu unatoa ujumbe gani ,tunaomba tueleze ujumbe uliomo kwenye wimbo huu ni unyenyekevu mbele za Mungu.Umetungwa kwa kuzingatia kwamba kama wanadamu kuna mara nyingi tunamkosea sana Mungu.
"Hivyo ni wimbo ambao ni ombi la kumuomba Mungu kuendelea kufinyanga na kutengeneza upya mioyo yetu hata pale tunapokosea au kutenda dhambi sana. Kwa kuwa Mungu siku zote ni Mungu wa huruma.
"Tuna imani wimbo huu utaendelea kuleta Watu Karibu na Mungu hata pale wanapojihisi ni wadhambi sana,"umesema uongozi wa kwaya hiyo ambayo imejizolea umaarufu kutokana na aina ya ujumbe unatolewa kupitia nyimbo zake mbalimbali.
0 Comments