Ticker

6/recent/ticker-posts

DED TEMEKE ATEMBELEA BANDA LA MANISPAA YA TEMEKE KWENYE MAONESHO NANENANE MKOANI MOROGORO



*************************

NA MWANDISHI WETU

MKURUGENZI wa Manispaa ya Temeke Ndg.Elihuruma Mabelya amevutiwa na namna banda la Halmashauri ya Temeke ambavyo limeweza kukusanya wajasiriamali wengi wa kutosha pamoja na shughuli zinazofanywa na Halmashauri ya Temeke katika Maonesho ya Nanenane Kanda ya Mashariki mkoani Morogoro

Amesema wajasiriamali hao ni wanufaika wa mkopo wa asilimia 10 na ni watu ambao wamekuwa wakijituma na wakotayari kuisaidia serikali kuhakikisha kwamba maisha yao wenyewe yanakuwa bora lakini maisha yanayowazunguka kwa maana ya familia yanakuwa bora na hatimae kuweza kuripa kodi kwa serikali.

"Mwaka huu wa fedha ambao tunaanza nao, moja kipaumbele chetu katika eneo hili la mikopo kwa asilimia 10 kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu ni kuhakikisha kwamba tunatoa elimu ya namna ya kufanya biashara lakini namna ambavyo vikundi hivi vinaweza kusimamia miradi yao na kurejesha". Amesema Ndg.Mabelya.

Aidha amesema kuwa ni wajibu wao kama halmashauri kulea vikundi hivyo, wanapokopesha lazima wawe walezi kwenye vikundi hivyo ili vilete manufaa kwa jamii, vilete marejesho yao ambayo yatabadilika kuwa mkopo kwa vikundi vingine.

Pamoja na hayo amewataka Wananchi wa Manispaa ya Temeke kupitia vikundi na maandiko ambayo watakuwa wameyaandika na kupitishwa na idara ya Maendeleo ya Jamii waje wakope mikopo hiyo kwasababu ipo kisheria ili kupunguza umasikini

Post a Comment

0 Comments