Afisa Mwendeshaji Mkuu wa Azam Tv Ltd Bw.Loth Mziray akizungumza katika Mkutano na waandishi wa habari wakati akitangaza kupungua kwa bei ya kisimbuzi cha digitali kinachotumia antenna (DTT) kuazia hapo kesho Septemba mosi mwaka huu,Meneja mauzo na usambazaji Adamu ndimbo akizungumza
*********************
Na Emmanuel Kawau.Dar es salaam.
Afisa mwendeshaji mkuu wa Azam Tv Ltd Loth Mziray amesema wanayonia madhubuti ya kuwafikia wananchi wote wa mijini na vijijini na kuhakikisha wanainamarisha maudhui kwa kutoa bidhaa bora na za kisasa ili kusambaza burudani kwa wote na kwa gharama nafuu.
Hayo ameyasema leo katika Mkutano na waandishi wa habari wakati akitangaza kupungua kwa bei ya kisimbuzi cha digitali kinachotumia antenna (DTT) kuazia hapo kesho Septemba mosi mwaka huu, Kutoka Shilingi elfu 99,000/= hadi Shilingi elfu 79,000/= ukinunua kisimbuzi kamili na antenna yake,huku ukinunua kisimbuzi bila antenna bei imeshuka kutoka Shilingi elfu 85,000/= hadi shilingi elfu 59,000/=na bei hizo ni kwa nchi nzima.
Aidha amesema kuwa wameongeza mikoa 6 ambayo itaweza kupata huduma ya kisimbuzi cha Antenna na kufanya jumla ya mikoa 17 yenye huduma hiyo katika kipindi cha mwaka mmoja na nusu.
"Kama wadau mnavyojua ndani ya mwaka mmoja na nusu tuliweza kufikia mikoa 11 hapa nchini ambayo ni Dar es Salaam,Dodoma,Morogoro,Tanga,Mtwara,Mbeya,Mwanza,Mara,Arusha, Kilimanjaro na shinyanga,
"Na sasa basi tunaenda kushusha mzigo wa kisimbuzi cha Antenna kwenye mikoa sita ambayo ni Kigoma mjini,Lindi mjini,Sumbawanga mjini, Wilaya ya tunduru iliyopo mkoani njombe,Tabora mjini,Wilaya ya makambako mkoani njombe mikoa mikoa hiyo itaanza kupata huduma rasmi kuanzia Septemba mosi mwaka huu,yaani kesho, lakini izingatiwe kuwa bei ya Kisimbuzi cha dishi bado bei yake ni ilele ya Shilingi 160,000/=" Alisema mziray
Kwa upande wake Meneja mauzo na usambazaji Adamu ndimbo amesema kuanzia kesho Septemba mosi kutakuwa na kampeni kabambe katika mkoa wa Dar es Salaam ambapo watazunguka jiji kusambaza visimbuzi kwa wateja kwa kushirikiana na mawakala huku kukifwatiwa na mfulilizo wa kampeni hiyo katika mikoa mingine hususani katika mikoa mipya.
"Wataje pia wanaweza kupata huduma kwa kupiga simu huduma kwa wateja namba 0784-108000 au kwa kufika kwa mawakala wa Azamu Tv waliopo karibu nao" Alisema Ndimbo.
0 Comments