**********
Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb), amefanya mazungumzo na Bi. Michelle Bachelet, Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa (UN) kwa ajili ya kubadilishana mawazo juu ya masuala ya haki za binadamu ikiwemo kutolea ufafanuzi tuhuma kuhusu Pori Tengefu la Loliondo na Hifadhi ya Ngorongoro.
Mazungumzo hayo yamefanyika jana tarehe 15 Julai 2022, Geneva Uswisi.
Kwa upande wake, Bi. Bachelet ameshukuru na kupongeza kwa namna ambavyo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inavyotekeleza masuala ya haki za binadamu hususan chini ya Serikali ya Awamu ya Sita, inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Katika mkutano huo Dkt. Ndumbaro aliambatana na Mhe. Maimuna Tarishi, Balozi wa Tanzania Nchini Uswisi na Mhe. Hoyce Temu Balozi Msaidizi
0 Comments