KAIMU Mrajis wa Vyama vya Ushirika Tanzania Juma Mokili ambaye pia ni Mkurugenzi wa Utafiti na Mafunzo kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania akizungumza wakati alipomuwakilisha Mrajis wa Vyama vya Ushirika Benson Ndiege wakati wa kufunga mafunzo ya Menejmenti ya vihatarishi kwa warajis wasaidizi wa Mikoa katika vyama vya ushirika, mafunzo hayo yamefanyika Jijini Dodoma.
Mkaguzi Mkuu wa ndani wa serikali msaidizi wa vihatarishi, mifumo na udhibiti wa ndani kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Abraham Msechu akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya warajis wasaidizi wa Mikoa yaliyofanyika Jijini Dodoma kwa lengo la kuwajengea uwezo kuhusu Menejmenti ya vihatarishi katika taasisi hiyo.
Mkaguzi Mkuu wa ndani kutoka tume ya maendeleo ya ushirika Tanzania bi. Mwanaidi Kalela akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya warajis wasaidizi wa Mikoa yaliyofanyika Jijini Dodoma kwa lengo la kuwajengea uwezo kuhusu Menejmenti ya vihatarishi katika taasisi hiyo.
Baadhi ya warajis wasaidizi wa Mikoa walioshiriki mafunzo hayo wakifuatilia matukio wakati wa kufunga mafunzo ya warajis wasaidizi wa Mikoa yaliyofanyika Jijini Dodoma kwa lengo la kuwajengea uwezo kuhusu Menejmenti ya vihatarishi katika taasisi hiyo.
KAIMU Majis wa Vyama vya Ushirika Juma Mokili wa pili kutoka kushoto waliokaa akiwa katika picha ya pamoja na wawezeshaji wa mafunzo hayo mara baada ya kufunga mafunzo ya warajis wasaidizi wa Mikoa yaliyofanyika Jijini Dodoma kwa lengo la kuwajengea uwezo kuhusu Menejmenti ya vihatarishi katika taasisi hiyo.
KAIMU Mrajis wa Vyama vya Ushirika Juma Mokili wa pili kutoka kushoto waliokaa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya warajis wasaidizi wa Mikoa mara maada ya kufunga mafunzo ya warajis wasaidizi wa Mikoa yaliyofanyika Jijini Dodoma kwa lengo la kuwajengea uwezo kuhusu Menejmenti ya vihatarishi katika taasisi hiyo.
.........................................
Na Alex Sonna– DODOMA
Tume ya Maendeleo ya Ushirika imewataka warajis wasaidizi wa Mikoa yote hapa nchini kuhakikisha wanaandaa mfumo madhubuti wa manejmenti ya vihatarishi katika ofisi zao ili kuandaa mipango ya tume na kufanya maamuzi ya kimkakati yanayotekelezeka katika majukumu ya kila siku.
Hayo yamebainishwa Jijini Dodoma na Kaimu mrajis wa Vyama vya Ushirika Juma Mokili ambaye pia ni Mkurugenzi wa Utafiti na Mafunzo kutoka tume hiyo wakati alipomuwakilisha Mrajis wa Vyama vya Ushirika Benson Ndiege wakati wa kufunga mafunzo ya Menejmenti ya vihatarishi kwa warajis wasaidizi wa Mikoa katika vyama vya ushirika.
Amesema ili kupanga mipango inayotekelezeka katika tume hiyo ni lazima kuhakikisha wanazuia kila viashiria vya menejmenti ya vihatarishi katika mipango yao.
“Kama mnavyofahamu tuko hapa kwa ajili ya kuhudhuria mafunzo ambayo yatatujengea uelewa na kutuwezesha kuanzisha na kusimamia mifumo ya menejmenti ya vihatarishi katika ofisi zetu” amesema Mokili.
Ameongeza kuwa “ Mafunzo haya yanafanyika kwa mujibu wa maelekezo yaliyomo kwenye muongozo wa kuanzaa fremu ya menejmenti ya vihatarishi katika taasisi za serikali uliotolewa mwaka 2012 na Wizara ya Fedha na mipango kupitia idara ya mkaguzi wa ndani” amesema.
Amesema lengo la muongozo huo ilikuwa ni kutoa dira ya uanzishwaji na utekelezaji wa mfumo menejmenti ya vihatarishi katika taasisi za serikali na kubainisha kuwa kwa mujibu wa mwongozo tume inatakiwa kuandaa fremu ya menejmenti ya vihatarishi, daftari la orodha ya vihatarishi ili kuwa na mfumo imara na kufikia malengo.
Amesema mafunzo hayo ni endelevu na kwa awamu ya pili yatafanyika kwa maafisa ushirika wa wilaya kwa lengo la kusimamia vihatarishi katika maeneo yao kwa kushirikiana wa warajis wasaidizi wa Mikoa yao na menejmenti ya tume.
“Mafunzo hayo yanafanyika ili kuweka misingi bora ya utekelezaji wa mwongozo wa vihatarishi lengo likiwa ni kuwaandaa waratibu menejmenti ya vihatarishi kuchukua jukumu la kuiongoza tume katika uanzishwaji na utekelezaji wa mfumo wa menejmenti ya vihatarishi” amesema.
Kwa upande wake Mkaguzi Mkuu wa ndani katika tume ya maendeleo ya ushirika Tanzania Bi. Mwanaidi Kalela amesema mafunzo hayo ni ya siku mbali na wamejifunza dhana ya vihatarishi, sifa ya vihatarishi na namna ya kuibua vihatarishi katika maeneo yao ya kazi.
“Tunaamini mafunzo haya yamekuwa ya tija na kutakuwa na mabadiliko makubwa katika utendaji kazi kwa kuwa wamejifunza muundo muzima wa vihatarishi katika taasisi zao” amesema.
0 Comments