Mkuu wa Mkoa wa Singida,Dk.Binilith Mahenge (katikati) akiongoza kikao cha wakulima, wasindikaji, viongozi wa vyama vya ushirika,Wakuu wa Wilaya,Wakurugenzi wa Halmashauri na wataalam wa kilimo kutoka wilaya zote za mkoa huo kilichofanyika mwishoni mwa wiki. Kutoka kushoto ni Katibu Tawala Msaidizi anayeshughulikia uzalishaji na uchumi, Stanslaus Choaji na Katibu Tawala Mkoa Singida, Dorothy Mwaluko.
Mwenyekiti wa AMCOS Kijiji cha Misughaa, Shaban Rajabu akizungumza kwenye kikao hicho.
Hamisi Samade kutoka wilayani Itgi akizungumza kwenye kikao hicho.
Taswira ya kikao hicho.
Kikao kikiendelea.
Kikaohicho kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea. Kutoka kulia ni Katibu wa AMCOS kutoka Kijiji cha Sambaru, Francis Kimanda, Afisa Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika Wilaya ya Ikungi, Msemo Gurisha na Afisa Mazao Wilaya ya Ikungi, Abdallah Sima.
Mkulima Yesaya Ambayuu kutoka Wilaya ya Itigi akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Mwakilishi kutoka Kiwanda cha kuchakata alizeti cha Maunt Meru akichangia jambo kwenye kikao hicho.
**********************
Na Dotto Mwaibale, Singida.
WAKULIMA wa Alizeti Mkoa wa Singida wameiomba Serikali kupima udongo katika wilaya zote kubaini aina gani ya mbegu ya alizeti inaweza kustawi vizuri na kutoa mavuno mazuri ili kuepukana tatizo la wakulima kupata hasara kutokana na kupewa mbegu zisizofaa.
Walisema hayo wakati wa kikao cha wakulima, wasindikaji, viongozi wa vyama vya ushirika,Wakuu wa Wilaya,Wakurugenzi wa Halmashauri na wataalam wa kilimo kutoka wilaya zote za mkoa huu kilichofanyika mwishoni mwa wiki.
Kikao hicho kilikuwa mahsusi kwa ajili kujadili mstakabali wa kilimo cha zao alizeti hasa ikizingatia mkoa wa Singida ni kati ya mikoa mitatu ambayo mikakati na serikali kulima alizeti kwa wingi ili kuongeza uzalishaji wa mafuta ya kula nchini. mikoa mingine ni Dodoma na Simiyu.
Walisema mbegu aina ya standard waliyopewa wakulima mkoa wa Singida katika msimu wa 2021/2022 imewatia hasara kubwa kutokana na baadhi ya maeneo kutostawi na hivyo kiwango cha uzalishaji wa alizeti kushuka sana.
"Wizara ya Kilimo ilipokuwa inatoa mbegu hizi kwa sisi wakulima kwani haikuona kuwa hazifai hadi imesababisha tumepata hasara kiasi hiki," alisema Milangton Musa mkulima kutoka Wilaya ya Mkalama.
Mkulima Hamis Said kutoka Wilaya ya Ikungi, alisema mpango wa serikali ulikuwa mzuri sana kuletewa mbegu ya ruzuku lakini tulicholetewa sio mbegu bali ni chakula.
"Hii tuliyoletewa ilikuwa sio mbegu kabisa, imetuongezea umaskini mkubwa wakulima nadhani hili lilifanyika kama kufunika kombe mwanaharamu apite," alisema.
Aidha, wakulima waliiomba serikali kabla ya kutoa mbegu ipime kwanza ardhi kila wilaya ili kujua udongo gani unafaa kwa kilimo cha alizeti na pia iongeze maafisa ughani wawepo kila kata.
Awali Mkuu wa Mkoa wa Singida,Dk.Binilith Mahenge, alisema mwaka jana mkoa uliweka mkakati kuongeza uzalishaji wa zao la alizeti kutokana na mahitaji ya matumizi ya mafuta ya kula nchini.
Alisema katika msimu huu wa 2021/2023 mkoa ulilenga kulima ekari 653,382.8 za alizeti ambapo serikali ilitoa tani 453.6 ambazo ziligawiwa kwa wakulima katika halmashauri zote za mkoa huu.
Dk.Mahenge alisema katika ekari hizo matarajio yalikuwa ni kuvuna tani 513.38 lakini bahati mbaya kutokana na changamoto ya mvua kunyesha chini ya wastani uzalishaji utapungua na kufikia tani 272.
Katibu Tawala Mkoa Singida, Dorothy Mwaluko, alisema mkoa unazo kata 139 hivyo itahakikisha maafisa ughani wanapelekwa katika kata zote.
Awali Katibu Tawala Msaidizi anayeshughulikia uzalishaji na uchumi, Stanslaus Choaji, alisema katika msimu wa 2021/2023 mkoa umejipanga kulima ekari 627,391 za mashamba ya alizeti.
0 Comments