Mwenyekiti wa Ccm Wilaya ya Pangani Abdarahman Abdallah akikabidhi fomu kwa Katibu Msaidizi wa Ccm Mkoa wa Tanga Kumotola Kumotola katika ofisi za Ccm.
Katibu Msaidizi Kumotola akimfuatilia Mwenyekiti Abdarahman wakati akijaza fomu.
*******************
Na Hamida Kamchalla, TANGA.
MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi Ccm Wilaya ya Pangani Rajabu Abdarahman Abdallah leo amechukua fomu ya kuwania Uenyekiti wa Ccm Mkoa wa Tanga akiminyana na Henry Daffa Shekifu anayetetea wadhifa wake.
Abdallah amechukua na kurejesha fomu hiyo huku Shekifu anayemaliza muda
wake akiwa ameshakamilisha mchakato huo siku moja mbele yake ikiwa ni
sehemu ya demokrasia na kutimiza haki ya kuomba kuteuliwa ndani ya Ccm.
Baadaa ya kurejesha fomu hizo zilizopokelewa na Kaimu Katibu wa Ccm Mkoa wa Tanga Kumotola Kumotola, Mwenyekiti huyo wa Ccm Pangani amesema ameingia kwenye kinyang'anyiro ikiwa sehemu ya kutimiza Demokrasia.
Amesema ndani ya Chama cha Mapinduzi Demokrasia ni kubwa na kila mwanachama anayo haki ya kuchagua na kuchaguliwa huku akibainisha kuwa baada ya zoezi lake hilo anakiachia chama kuendelea na taratibu zake.
"Ndani ya Ccm Demokrasia ni kubwa, kila Mwanachama ana haki ya kuchagua na kuchaguliwa na hivyo nami nimefanya kama ilivyo kwa Wanachama wengine, tuombe Mungu chama kiendelee na taratibu zake" amesemasema Abdallah.
Kitendo cha Mwenyekiti huyo wa Ccm Wilaya ya Pangani kuchukua fomu ni
kinaweza kutafsiriwa kama kupanda kwa joto la uchaguzi ndani ya Ccm katika
kipindi ambacho Shekifu ameonesha nia ya kutetea wadhifa wake huo.
0 Comments