Ticker

6/recent/ticker-posts

TUCTA WAOMBA NYONGEZA YA MISHAHARA ITAZAMWE KWA ASILIMIA SIYO KIWANGO CHA MSHAHARA.



***************************

Na Zena Mohamed,Dodoma.

SHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA)limeomba nyongeza ya mishahara itazamwe kwa kuangalia asilimia na sio kiwango cha mshahara wa Mtu wakidai kuwa kila mtumishi anahaki ya kupata mshahara mzuri kulingana na kazi yake.

TUCTA limewasilisha serikalini hoja kimaandishi ikiwemo nyongeza ndogo ya mshahara iliyoongezwa huku ikiiomba serikali kuangalia upya suala hilo.

Akizungumza na Waandishi wa habari jijini hapa jana mara baada ya kukabidhi hoja hizo Rais wa TUCTA Tumaini Nyamhokya amesema kuwa mambo ya msingi waliyoyazingatia katika wasilisho hilo ni pamoja na namna ya nyongezaya mishahara ilivyofanyika kwani utaratibu umekuwa ambao haukumridhisha mtumishi yeyote wa umma aliyepewa nyongeza hiyo ya mshahara.

Amesema kuwa kiwango cha kima cha chini ni asilimia 23.3 lakini ukiangalia kima cha juu tumeona tofauti yake kaongezwa asilimia 0.6,ni tofauti kubwa mno ambayo haijawahi kutokea na huwa utaratibu wa namna hii haufanyiki.

“Tukumbuke Rais alilenga kuongeza mishahara nahakuwa amelenga kuwatoa watu wa daraja Fulani kuwapeleka mahala pengine,kwahiyo tunaamini kama ningazi ya mshahara tunaamini inagusa kila ngazi ya mshahara kwa utumishi wa umma”amesema Nyamhokya.

Ametaja hoja nyingine kuwa ni pamoja na nyongeza ya mshahara kuna baadhi ya kada hazikuguswa ,baadhi ya taasisi za umma hazikuguswa kama vile watumishi wengi wenye mishahara binafsi,lakini kwenye mishahara binafsi kuna wale ambao wamemaliza darasa la saba wanasema kwamba kwenye mfumo wa serikali hawasomeki kabisa .

“Lakini pia ukiangalia kwenye kada kama za idara ya afya ,idara ya utawala kwa hawa watendaji wa kata na mitaa nao hawakupata nyongeza ya mshahara kabisa,hivyo hatuoni sababu ni nini ambayo imefanya watu hawa wasiongezewe mishahara,"amesema.

Aidha amesema pia kuna baadhi ya taasisi kama ATCL,TTCL,TRC hawa nao hawajaguswa wakati na wenyewe ni sekta ya umma kwahiyo wanaona jambo hili halijakaa vizuri ndio maana wamewapa hoja hizo serikali wakazifanyie kazi.

"Kiwango cha elfu 70 bado siyo kuwango halisia cha kumtoa mtumishi kwenye adha za maisha ukilinganisha na maisha ghali yaliyopo sasa hivyo siyo kwamba wamerizika na hiyo elfu 70 bado wanahitaji iongezeke zaidi,

“Tutizame zaidi asilimia badala ya kuangalia kiwango cha fedha ,tofauti ya 23.3 kwakiwango cha chini cha mshahara na asilimia 0.6 kwa kiwango cha juu tumeona imepungua mno imekwenda kwanye mtu anayekwenda kwenye 0 hivyo tumependekeza mtu mwenye kima cha juu asipungukiwe nyongeza ya asilimia 15 wakati mwenye kima cha chini ameongezewa asilimia 23.3 ya mshahara”amesema.

Hata hiyo Nyamhokya amesema kuwa baada ya kuwasilisha hoja hizo wanasubiri majibu ya serikali ili waone watakuja na kitu gani kwani jambo hilo siyo la muda mrefu.

Post a Comment

0 Comments