Ticker

6/recent/ticker-posts

TIRDO YABUNI TEKNOLOJIA YA KUONGEZA THAMANI YA TAKA ZITOKANAZO NA MAZAO

Mtafiti wa Shirika la Utafiti na Maendelea ya Viwanda (TIRDO) Bi.Jacqueline Mwandwa akimuelezea jambo Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Jumanne Sajini (Mb.) mara baada ya kutembelea banda la TIRDO akiwa na Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe Dkt.Ashatu Kijaji pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji, Viwanda, Biashara Prof. Godius Kahyarara katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Sabasaba yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam. Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe Dkt.Ashatu Kijaji (mwenye ushungi) akiuliza jambo kwa Mtafiti wa Shirika la Utafiti na Maendelea ya Viwanda Tanzania (TIRDO) Bi.Jacqueline Mwandwa mara baada ya kutembelea banda la TIRDO katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Sabasaba yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Jumanne Sajini (Mb.)

*************************

WAZIRI wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe Dkt.Ashatu Kijaji ameipongeza Shirika la Utafiti na Maendelea ya Viwanda (TIRDO) kwa kuendelea kuibua tafiti mbalimbali hasa kwa kuongeza thamani taka zitokanazo na mazao na kufanya kuwa fursa kwa wajasiriamali.

Waziri Kijaji ametoa pongezi hizo leo Julai 2,2022 mara baada ya kutembelea banda la TIRDO katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Sabasaba yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza kwenye Maonesho hayo Kaimu Mkurugenzi upande wa Tehama-TIRDO Bi.Elizabeth Mtegwa amesema katika maonesho hayo TIRDO wamekuja na teknolojia ya kuongeza thamani katika taka zitokanazo na mazao ambapo wamekuja na maganda ya machungwa ambayo wameyakausha kisha wakayasaga na kuweza kuyakamua kwa mashine maaluumu na kupata mafuta yatokanayo na maganda hayo (Mafuta tete).

Amesema mafuta hayo yanamatumizi mbalimbali ikiwemo ni malighafi kwenye viwanda vinavyotengeneza pafyumu, mafuta, sabuni lakini pia yanaweza kutumika kwa matumizi ya nyumbani kwa maana ya kuongeza radha katika vyakula pamoja na kutumika katika masaji.

"Mafuta haya yanaviashiria kuzuia kuzeeka, kwahiyo ukitumia kwa kuchanga na mafuta ambayo unapaka nyumbani na kutumika kila siku unafanya ngozi yako kuwa laini na yakuvutia". Amesema Bi.Mtegwa.

Aidha Bi.Mtegwa amesema teknolojia hiyo sio kwenye maganda peke yake, unaweza ukatoa mafuta hayo kwenye mchaichai, iriki, mdarasini na hata miti kama mwarobaini kwahiyo soko lake lipo hivyo watanzania wanatakiwa kuchangamkia fursa hiyo.

Post a Comment

0 Comments