Mwenyekiti Taifa wa Taasisi ya kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere,Paul Kimiti akizungumza na Waandishi wa habari nyumbani kwake jijini Dar es salaam kuhusu kuhamasisha wananchi kujitokeza kwenye zoezi la sensa agosti 23 mwaka.
***************************
Na Magrethy Katengu
Mwenyekiti Taifa wa Taasisi ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Paul Kimiti ametoa rai kwa watanzania kujitokeza kwa wingi kushiriki zoezi la sensa litakalofanyika agost 23 mwaka huu ili kusaidia serikali kupata takwimu sahihi nakuweza kugawanya rasilimari zilizopo kwa uwiano sahihi.
Kimiti ametoa rai hiyo jijini Dar es salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kwa ajili yakuhamasisha wananchi kujitokeza kuhesabiwa lakini pia kuendeleza falsafa za baba wa Taifa hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambaye enzi ya uhai wake alihimiza amani,upendo,mshikamano,pamoja na maendeleo.
Amesema kwamba yeye kama Mwenyekiti Taifa wa Taasisi ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere anatamani kuona zoezi la sensa linafaniliwa kwani ndio msingi wa kiweza kulifanya Taifa kuweza kupanga dira ya Mandeleo Kwa wananchi wake.
" Rais Samia hawezi kufanya kazi peke yake lazima tumsaidie,kujua idadi ya watu na maendeleo yao ni jambo muhimu sana,hivyo tusivuruge zoezi la sensa bali tuhakikishe linafanikiwa na Nchi yetu kupitia Wizara mama ambayo ni Wizara na Fedha na Mipango iweze kutekeleza mipango yake.
Kimiti ambaye amewahi kutumikia nyadhifa mbalimbali hapa nchini ikiwemo Wizara ya Kilimo katika serikali ya awamu ya tatu hayati Benjamini Mkapa, ameongeza kuwa sensa ndio uchumi wa Taifa,hivyo amewaagiza viongozi wa taasisi hiyo kuanzia ngazi ya mkoa,wilaya, hadi Kata kuendelea kuwaelimisha wananchi kujitokeza kuhesabiwa.
"Kwa vile tuaingia katika mchakato wa kuendeleza makongamano ya kuenzi miaka 100 ya Mwalimu Nyerere hadi mwezi April mwakani(2023) naagiza agenda kubwa iwe sensa,viongozi wajikite kuzungumzia sensa,pili wazungumze falsafa ya Mwalimu Nyerere ambaye alipigania nchi iwe na amani,utulivu,na mshikamano" amesema.
Nakuongeza " Mwezi april mwaka huu tulizindua rasmi taasisi yetu nakupeana maagizo yakuendelea na makongamano yakumuenzi baba wa Taifa ,hivyo tutumie utaalamu tulio nao kwenye mikoa au wilaya zetu kumuenzi Mwalimu Nyerere,nisingependa kuona falsafa za baba wa Taifa zinapotea.
0 Comments