Ticker

6/recent/ticker-posts

MSALABA MWEKUNDU WASAIDIA KAYA 1200 ZA KIFUGAJI ZILIZOATHIRIKA KWA UKAME MANYARA NA ARUSHA



*************

Na Mwandishi Wetu,

CHAMA cha Msalaba Mwekundu nchini (Tanzania Red Cross Society-TRCS), kimeweza kutoa msaada kwa Kaya 1200 za kifugaji zilizoathirika kwa ukame katika mikoa ya Manyara na Arusha.

Ambapo TRCS hadi kufikia sasa tayari imeshatoa msaada wa kifedha kiasi cha Millioni 216 kwa kaya hizo,1200,

Rais wa TRCS, ambaye pia ni Mbunge wa Mufindi Kusini, Mhe. David Mwakiposa Kihenzile amebainisha hayo katika Kijiji cha Donyonadoo katika Jimbo la Monduli mojawapo ya vijiji vilivyoathiriwa na ukame huo kwa kiasi kikubwa,

Alisema TRCS na Serikali wameguswa na jambo hilo na kuweza kutoa msaada huo wa kibinadamu ikiwemo vitu, madawa na fedha hizo.

Ambapo katika zoezi la Ugawaji wa Fedha hizo amesema wamejikita hasa kutoa Misaada ya kibinadamu kabla na baada ya Maafa, Ambapo Msaada huo unalenga Kaya zilizoathirika na Maafa ya Mifugo Mwaka jana.

Aidha, katika tukio hilo akiongozana na mwenyeji wake Mbunge wa jimbo la Monduli, Mh. Fredrick Lowassa, alisema TRCS kimetoa msaada wa kiasi cha Shilingi 210,000 katika kaya 114 zilizopelekea jumla ya shilingi Milioni 23 kugawiwa kwa wanakijiji hawa ili kusaidia kujikimu na kupunguza makali ya athari wa ukame huo.

Mh. Kihenzile ameongeza kuwa, Wanagusa Familia zilizoathirika na Ukame, Ambapo jumla ya vifo vya Mifugo ni Punda zaidi ya elfu 2 Ng’ombe zaidi ya elfu 41,Mbuzi zaid elfu 34, na Kondoo zaidi ya elfu 54, kwa Wilaya ya Monduli, na kusema pamoja na kutoa Fedha taslim.

Pia wametoa vyombo vya kuhifadhia maji ya nyumbani, dawa za kutibu maji (vidonge), chakula lishe kwa watoto wenye utapiamulo, elimu ya kupinga ukatili na umuhimu wa shule kwa mtoto wa kike.

Mh.Kihenzile amewataka wananchi wa Donyonadoo kuwa wanachama na voluntia wa TRCS kwani yapo mambo ambayo watanufaika nayo kwakusaidiana wao kwa wao ikiwemo mafunzo ya huduma ya kwanza na

wasiishie kuitambua TRCS kam chombo cha kuwasiaida waathirika na wahanga tu bali watambue yakuwa Red Cross popote Duniani inajengwa na watu wanaojitolea kwaajili ya watu wengine kwani hata msaada huo walioupata wapo watu kutoka nchi mbali mbali kupitia IFRC wamejitolea kwaajili yao ili kuwapunguzia maumivu kwa madhira walioyoyapata.

Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo hilo la Monduli, Mh.Fredrick Lowassa amemshukuru Rais wa TRCS kwa Kufika Idonyonaado, na kusema mchakato huo ni wa kitaalamu, Miundombinu ya idonyonaado ni changamoto kupatikana kwa maendeleo hivyo anawashukuru sana TRCS chini ya uongozi wa Mh.Kihenzile kwakuweza kuwafikia wananchi hao

Ambapo amebainisha kuwa, sio rahis kila mtu kuwafikia nakuomba TRCS iendelee kuwa karibu nao kwani wamesitiriwa kiasi kwamba wote wanaridhia kuwa mabalozi wazuri wa Red Cross.

Aidha, Mh.Fredrick Lowassa amekiri kutambua mchango mkubwa walioutoa nakuwaomba wasiiishie hapo kwani TRCS ni kisaidizi cha Serikali kama ambavyo inajulikana hivyo basi waendelee kuwa bega kwa began a serikali ya awamu ya sita chini ya Samia Suluhu Hassani kuhakikisha jamii zote zipo salama.

Post a Comment

0 Comments