*******************
Na Hamida Kamchalla, TANGA.
KAMISAA wa Sensa ya Watu na Makazi 2022, Anna Makinda amesema ili serikali iweze kupanga mipango yake kwa ufasaha na kuondokana na tatizo la upungufu wa mahitaji muhimu ya wananchi no lazima watu wote wahesabiwe.
Makinda ameyasema hayo katika mkutano wa viongozi wa dini kuhusu maandalizi ya sensa ambapo pia aliwasisitiza viongozi hao kuwakumbusha waumini wao misikitini na makanisani kuhusu umuhimu wa sensa na kwamba wajitokeze kwa wingi kuhesabiwa ifikapo Agosti 23 mwaka huu.
"Suala la upungufu wa mahitaji muhimu kwa wananchi kama vile madawati mashuleni lilikuwepo kwasababu tulikuwa hatujui tuko wangapi, tumeongezeka kwa kiwango gani na watoto wetu wamezaliwa kwa kiwango gani,
"Lakini kwa sensa hii, tukishamaliza kabisa tutajua idadi kamili ya watu majumbani, tutajua mtoto ambaye anazaliwa leo baada ya miaka mitatu atatakiwa kuanza shule ya awali, na baadaye kuendelea na elimu nyingine, kwahiyo serikali kipindi hiki chore inajua kabisa mwaka huu wameongezeka watoto wangapi, inajiandaa" amesema.
Aidha amebainisha kwamba serikali ikiwa na uhakika wa takwimu sahihi ya wananchi inaweka mambo sawa, na kutafuta rasilimali za kuweza kumudu wananchi kabla ambapo pia matumizi ya vyanzo vya fedha vanatumika vizuri.
"Hii shuhuli ya kutengeneza vitu kidharura dharura kwakweli inaleta matatuzi hata thamani ya vitu inakuwa chini, rushwa inakuwepo kwasababu ya haraka, lakini kumbe tukiwa na mipangilio iliyitulia kabisa, tunajua watu kadhaa watakuwa kidato cha kwanza mwaka huu, na vitu vingine kama hivyo" amebainisha Makinda.
"Sensa ni kitu ambacho kinaipa serikali ubora wa kufanya kazi zake na sensa ya mwaka huu ni tofauti kabisa ndiomaana nasema tunakaribia kufika watu milioni 64 mwaka huu kutokana na uzazi tulioupata mwaka 2012, tulikuwa tumeongezeka kwa asilimia 2.9, kwahiyo ndiyo tuliyofanyia hesabu" amesema.
Kwa upande wake mkuu wa Mkoa wa Tanga Adam Malima amesema uelimishaji na uhamasishaji wa sensa ya watu na makazi vimekuwa vikifanyika sana katika maeneo mbalimbali wanapotembelea za Mkoa kwa shuhuli za maendeleo wanapokutana na wananchi..
"Katika mikutano hiyo, tumekuwa tukiwaelimisha wananchi umuhimu wa sensa na wajibu wao katika kuifanikisha, halikadhalika kwa upande wa viongozi wa dini nap wamekuwa sehemu ya juhudi za serikali za kuelimisha imma kuhusu sensa na kuwaomba waumini na wananchi wa Mikoa yetu kushiriki sensa" amesema.
"Kwa mnasaba huo, sina budi kuwashukuru na kuwapongeza viongozi wa dini kwa kutimiza wajibu wao kwa jamii kwa kusaifia maendeleo ya nchi yetu kwakuwa sensa ndiyo msingi wa takwimu ambapo ndizo zinazotumika kupanga mipango ya maendeleo ya nchi yetu" amesema.
Hata hivyo Malima ametoa wito kwa viongozi hao na kuwaomba kutumia uongozi na mamlaka yao kwa wanaowaongoza, kwani ushawishi na ukaribu wao kwa waumini na jamii nzima, kuwaelimisha na kuwahamasisha kushiriki sensa kwakuwa ni msingi wa maendeleo yao wenyewe na nchi kwa ujumla.
"Tuwaelimishe wananchi kuwa rasilimali zinazotumika kupeleka huduma za jamii na uchumi katika maeneo yao wanayoishi zinategemea takwimu za idadi ya watu ambazo hutokana na sensa na takwimu nyingine zinazozalishwa nchini" amesema Malima.
"Kwa upande wa Mkoa wetu tunaendelea na maandalizi mbalimbali ya sensa ili iwe na mafanikio makubwa, mojawapo ya shuhuli tunayotarajia ni kuhakikisha watu wote waliolala usiku wa kuamkia tarehe 23 Agosti mwaka huu wanahesabiwa" amebainisha.
0 Comments