Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akipokea tuzo ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa mchango wake katika kukuza na kueneza lugha ya Kiswahili wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani iliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam leo tarehe 7 Julai 2022.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akizindua Kamusi Maalum kwaajili ya Shule za Msingi Pamoja na mkakati wa Taifa wa kubidhaisha ndani na nje ya nchi wa mwaka 2022-2032 wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani iliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam leo tarehe 7 Julai 2022.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akimkabidhi baadhi ya vitabu vya lugha ya Kiswahili Waziri wa Elimu ya Msingi wa Afrika Kusini Prof. Matsie Angelina Motshekga wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani iliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam leo tarehe 7 Julai 2022.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akizungumza na viongozi na wadau wa lugha ya Kiswahili kutoka ndani na nje ya nchi wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani iliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam leo tarehe 7 Julai 2022. Katibu Mkuu Wizara ya Utamduni, Sanaa na Michezo Dkt.Hassan Abbas akizungumza na viongozi na wadau wa lugha ya Kiswahili kutoka ndani na nje ya nchi wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani iliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam leo tarehe 7 Julai 2022. Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda akizungumza na viongozi na wadau wa lugha ya Kiswahili kutoka ndani na nje ya nchi wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani iliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam leo tarehe 7 Julai 2022. Waziri wa Elimu ya Msingi wa Afrika Kusini Prof. Matsie Angelina Motshekga akizungumza na viongozi na wadau wa lugha ya Kiswahili kutoka ndani na nje ya nchi wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani iliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam leo tarehe 7 Julai 2022.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akishuhudia utiaji Saini wa makubaliano baina ya Tanzania na Afrika Kusini juu ya ufundishaji wa lugha ya Kiswahili nchini Afrika Kusini wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani iliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam leo tarehe 7 Julai 2022.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akikagua mabanda mbalimbali ya walioshiriki maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani yaliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam leo tarehe 7 Julai 2022.Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akicheza mchezo wa Bao na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahman Kinana wakati alipotembelea Mabanda mbalimbali ya walioshiriki Maadhimisho Siku ya Kiswahili Duniani yaliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam leo tarehe 7 Julai 2022.
**************************
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango amezitaka Wizara zenye dhamana ya Elimu kufanyia kazi matokeo ya tafiti nyingi ambazo zimefanyika kuhusu lugha ipi inafaa kufundishia ili Serikali ifanye uamuzi na hatimaye watoto na vijana wa Kitanzania waanze kujifunza kwa lugha yao ya kiswahili kuanzia shule ya awali hadi Chuo Kikuu.
Makamu wa Rais amesema hayo wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani yaliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam.
Aidha amezitaka Wizara na taasisi za Serikali ziendelee kutekeleza maagizo ya Serikali yaliyokwishatolewa ambayo ni nyaraka za mawasiliano za Wizara na Idara zake ziwe kwa lugha ya kiswahili na kwamba mikutano, warsha, semina, mijadala ya umma na dhifa ziendeshwe kwa Kiswahili. Vilevile, majina ya barabara, mitaa, mabango, fomu za usaili na maelekezo ya matumizi ya dawa zote na bidhaa na huduma pia viandikwe kwa Kiswahili.
Makamu wa Rais ametoa wito kwa wataalam na mabingwa wa lugha ya kiswahili kuendelea kuongea kiswahili fasaha pamoja na kuandika vitabu vya taaluma mbalimbali kwa lugha hiyo ili kuendelea kukabiliana na ongezeko la upotoshaji wa matumizi ya lugha ya kiswahili miongoni mwa jamii, hususan vijana.
Amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ipo tayari kushirikiana na taasisi na wadau mbalimbali, kuhamasisha matumizi ya lugha ya Kiswahili na kujenga ushawishi kwa nchi nyingine kuingiza Kiswahili katika mitaala yao ili kuendelea kusambaza lugha hiyo adhimu kama ilivyoelekezwa katika Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya Mwaka 2020 – 2025.
Awali akisoma salamu kwa niaba ya Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO Tanzania) , mkuu wa kitengo cha Elimu katika shirika hilo Bi Faith Shayo amesema kuthamini lugha mbalimbali ni kipaumbele katika shirika la UNESCO.
Amesema lugha ya Kiswahili inayotoa fursa mbadala inayolenga kukidhi mtizamo wa dunia kwa ujumla.
Ameongeza kwamba Kiswahili ni kati ya lugha kumi zinazozungumzwa sana duniani na kujenga utengamano miongoni mwa jamii na mataifa mbalimbali.
Kwa Upande wake Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mohamed Mchengerwa amesema Wizara itaendelea kupokea maoni na ushauri wa wadau wa lugha ya Kiswahili ili kuhakikisha lugha hiyo inaendelea kuku ana kuenea duniani.
Mchengerewa ameongeza kwamba Wizara imelenga kuchagiza ujenzi wa chuo kikuu cha Kiswahili Dunia katika ardhi ya Tanzania.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda amesema Tanzania ni kinara wa Kiswahili fasaha hivyo watanzania wanapaswa kukuza, kutunza na kueneza Kiswahili fasaha.
Katika maadhimisho hayo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ametuma salamu kwa njia ya video akiwashukuru wote walitoa mchango wao katika kufanikisha kuipa heshima lugha ya Kiswahili hadi kupata siku maalum ya lugha hiyo duniani.
Amesema serikali imejipanga kueneza Kiswahili duniani kote ikiwemo kuziwezesha ofisi za kibalozi zilizopo nje ya Tanzania kuhamasisha uanzishwaji wa vituo vya kufundishia Kiswahili kwa wageni ambayo walimu wake watakuwa ni vijana waliohitimu vyuo vikuu vya Tanzania.
Rais Samia ameungana na Rais wa Jamhuri ya Msumbiji Mheshimiwa Filipe Josinto Nyusi na Rais wa Jamhuri ya Burundi Mheshimiwa Evariste Ndayishimiye ambao kwa pamoja wamepongeza juhudi za Tanzania katika kukuza na kueneza lugha ya kiswahili duniani.
0 Comments