Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango na mkewe Mama Mbonimpaye Mpango wakishiriki misa takatifu ya Upadirisho wa Mapadre sita wa kanisa katoliki Jimbo la Kigoma iliofanyika Parokia ya Mtakatifu Luka Kijiji cha Makere Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma leo tarehe 28 Julai 2022.
Askofu wa Jimbo la Kigoma Mhashamu Joseph Mlola akiwapa daraja la Upadre jumla ya Mapadre sita katika misa takatifu iliofanyika Parokia ya Mtakatifu Luka Kijiji cha makere Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma leo tarehe 28 Julai 2022.
Mapadri sita waliopata daraja hilo katika misa takatifu iliofanyika Parokia ya Mtakatifu Luka Kijiji cha makere Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma wakitoa baraka kwa waumini walioshiriki ibada hiyo leo tarehe 28 Julai 2022.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akizungumza na mapadre pamoja na waumini waliohudhuria misa takatifu ya upadirisho wa Mapadre sita wa Kanisa Katoliki Jimbo la Kigoma iliofanyika Parokia ya Mtakatifu Luka Kijiji cha Makere Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma leo tarehe 28 Julai 2022.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango na mkewe Mama Mbonimpaye Mpango wakiwa katika picha ya pamoja na Askofu wa Jimbo la Kigoma Mhashamu Joseph Mlola pamoja na Mapadre sita waliopata upadirisho katika misa takatifu iliofanyika Parokia ya Mtakatifu Luka Kijiji cha Makere Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma leo tarehe 28 Julai 2022.
**********************
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango na mkewe Mama Mbonimpaye Mpango leo tarehe 28 Julai 2022 wameshiriki ibada ya misa takatifu ya Upadirisho wa Mapadre sita wa kanisa katoliki Jimbo la Kigoma iliofanyika Parokia ya Mtakatifu Luka Kijiji cha Makere Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma.
Misa hiyo imeongozwa na Askofu wa Jimbo la Kigoma Mhashamu Joseph Mlola ikihudhuriwa na mapadre kutoka maeneo mbalimbali ya ndani na nje ya Kigoma pamoja na viongozi wa dini, serikali, vyama vya siasa na waumini mbalimbali.
Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa misa hiyo takatifu, Makamu wa Rais amewasilisha salamu za pongezi kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kanisa katoliki kupata mapadre sita wapya kwa wakati mmoja.
Makamu wa Rais amewaasa Mapadre hao kuwa kimbilio la waumini, kuwafundisha waumini kuwa na kiasi na busara kubwa itakayoponya na kuokoa roho za watu.
Amesema mapadre wanapaswa kujiepusha na sababu zozote za kulaumiwa pamoja na kushitakiwa kama yasemavyo maandiko katika biblia takatifu.
Aidha Makamu wa Rais amewasihi wananchi wa Kigoma na Tanzania kwa ujumla kutunza na kuhifadhi mazingira kwani uharibifu wake limekuwa tatizo kubwa na lenye athari mbaya sana kwa Taifa na dunia kwa ujumla.
Amesema serikali itachukua hatua kali zaidi kwa yeyote atakaejihusisha na uharifu wa mazingira ikiwemo kuchoma moto misitu pamoja na kuharibu vyanzo vya maji.
Pia Makamu wa Rais amewahimiza waumi hao kuhakikisha wanashiriki zoezi la sensa ya watu na makazi itakayofanyika tarehe 23 Agosti 2022.
Amesema takwimu zitakazopatikana katika zoezi hilo zitaisaidia Serikali kuweka mikakati bora na sahihi ya kuwafikishia maendeleo na mahitaji muhimu kama vile maji, shule, hospitali, barabara, umeme, ulinzi na Taasisi za utoaji haki.
Kwa upande wake Askofu wa Jimbo la Kigoma Mhashamu Joseph Mlola amewaomba waumini kuwaombea Mapadre hao ili waweze kutimiza majukumu yao kwa ufanisi pamoja na kubaki na hali ya kutangaza neno la Mungu siku zote.
Katika Misa hiyo Makamu wa Rais Dkt. Mpango amechangia shilingi milioni 10 kwaajili ya ujenzi wa kanisa la parokia hiyo.
0 Comments