Baadhi ya wananchi waliotembelea banda la FCC wakipatiwa huduma katika Maonesho ya 46 ya biashara ya kimataifa yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba Jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mkuu wa FCC Bw.William Erio akizungumza na waandishi wa habari katika Maonesho ya 46 ya biashara ya kimataifa yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba Jijini Dar es salaam
***************************8
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Tume ya ushindani Tanzania (FCC) imewataka wananchi kutembelea banda lao katika Maonesho ya 46 ya biashara ya kimataifa yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba ili waweze kupata huduma ikiwemo kufahamu bidhaa bandia na bidhaa halisi.
Akizungumza katika Maonesho hayo leo Julai 03, 2022 Mkurugenzi Mkuu wa FCC Bw.William Erio amesema wananchi ambao watapata fursa kupita katika banda lao wataweza kuzijua bidhaa hizo na waweze kulindwa kwa kupata bidhaa sahihi na zisizo bandia.
"Kwenye banda letu tutaonesha bidhaa mbalimbali bandia na bidhaa halisi, kwahiyo nitoe wito kwa wananchi ambao watapata fursa kutembelea maonesho haya wapite hapa ili waweze kuzijua bidhaa hizo na waweze kulindwa". Amesema
Amesema wamekuwa wakihakikisha makampuni yanayokuja nchini kwa nia ya kujiunga na makampuni mengine ili waweze kufanya biashara au uwekezaji wanapata vibali stahiki kutoka FCC jambo ambalo wamekuwa wakilifanya kwahiyo watu wote ambao wanataka kufika wasisite kutembelea banda lao kwenye maonesho ya 46 ya Biashara kwenye viwanja vya sabasaba.
Aidha amesema wamekuwa wakihakikisha mikataba kati ya walaji na wale waliotengeneza watoa huduma inakuwa ni vizuri kwao inawalinda na watapata huduma sitahiki katika taratibu ambazo hazitawagandamiza au hazitawaletea hasara.
"Wananchi kwa ujumla wapite kwenye banda la Wizara ya Viwanda na Biashara mbapo sisi tupo kwaajili ya kupata huduma nyingi pamoja na elimu ambazo FCC huwa tunatoa mara kwa mara katika ofisi zetu". Amesema Bw.Urio
0 Comments