Ticker

6/recent/ticker-posts

BAYPORT YAJA KIVINGINE KURAHISISHA HUDUMA KWA WATUMISHI WA UMMA

Balozi wa Taasisi ya fedha Bayport Haji Manara akizungumza na Waandishi wa habari .
Afisa Uendeshaji wa Bayport Ndelingo Materu akizungumza na Waandishi habari.

********************
Na Magrethy Katengu

Taasisi ya Kifedha ya Bayport imesema itahakikisha inasaidia Jamii kwa kurahisisha kwa kuwahudumia Watumishi wa Umma kuwapatia mikopo kwa riba nafuu kwa njia ya Mtandao popote walipo

Ameyasema hayo leo Dar es salaam Afisa Uendeshaji Mkuu Bayport Ndelingo Materi katika hafla ya utiaji saini Mkataba na Aliyekuwa Mhamasishaji klabu ya Yanga Afrikan Haji Manara kuwa Balozi wa taasisi hiyo ambapo ataitangaza kupitia mitandao yake ya kijamii ikiwemo akaunti zake za Instagram ,Twitter, Facebook,

Hata hivyo Afisa Uendeshaji Mkuu wa Bayport Ndelingo Materu amesema kwamba taasisi hiyo inatoa huduma za mikopo kwa watumishi wa Umma pekee,ambapo mikopo hiyo inatolewa kwa njia ya mtandao.

Bw.Materu amendelea kufafanua kuwa mteja anaetaka Mkopo anapaswa kupiga simu au kubonyeza *150*49# nakufuata maelekezo ya namna ya kukidhi vigezo vya kupata Mkopo,hivyo amesema kwamba hakuna haja yakusafiri muda mrefu au kuandika nyaraka zuomba Mkopo.


" Bayport inamrahisishia mteja kupata Mkopo Kwa njia ya haraka Kwa njia ya mtandao,leo tuna mtambulisha Khaji Manara kiwa Balozi wetu kwasababu tafikisha taarifa zetu Kwa wafuasi wengi wanaomfuatilia kwenye mitandao yake ya Kijamii ikiwemo Instagram , Tweeter, na Facebook, amesema Materu.


Kwa upande wake Haji Manara amesema kwamba mkataba huo atahakikisha anautendea haki kutokana na uwezo wake wa ushawishi kupitia mitandao ya Kijamii kwani taasisi hiyo ni kubwa na ipo kwa mujibu wa kisheria ina miaka 16 katika utoaji huduma ya fedha na inatoa mkopo ndani ya saa 24.


"Masharti ya Bayport siyo mwiba Kwa watumishi wa Umma ambao wanalipwa na serikali pamoja na taasisi zake,hivyo nawasihi wachangamkie fursa hii ,kwani upatikanaji wa mikopo yao ni rahisi sana na inalipwa kupitia simu ya kiganjani popote ulipo." Amesema Manara.


Aidha Khaji Manara ametumia fursa hiyo kuwakumbusha wachezaji wa mpira wa miguu wenye majina makubwa kutumia mitandao ya Kijamii Kwa ajili ya kujitangaza nakupata kipato kwani baadhi yao wamekuwa wakiachana na soka wanajikuta wanaishi maisha magumu.

Post a Comment

0 Comments