Ticker

6/recent/ticker-posts

BENKI YA CRDB YAKABIDHI PIKIPIKI 8 KWA WARAJISI WA USHIRIKA


Muonekano wa pikipiki nane (8) zenye thamani ya shilingi Milioni 24 .5 zilizotolewa na Benki ya CRDB kwa ajili ya warajisi kama nyenzo ya usafiri.
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Said Pamui (kulia) akimkabidhi Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe ufunguo wa Pikipiki ishara ya kukabidhi pikipiki nane (8) zenye thamani ya shilingi Milioni 24 .5 zitakazo kwenda kutumiwa na warajisi kama nyenzo ya usafiri.

Na Mwandishi wetu  - Malunde 1 blog
Benki ya CRDB imekabidhi pikipiki nane (8)zenye thamani ya shilingi Milioni 24 .5 zitakazo kwenda kutumiwa na warajisi  wa vyama vya ushirika kama nyenzo ya usafiri.

Akikabidhi pikipiki hizo Jumamosi Julai 2,2022 kwa Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe katika maadhimisho ya Siku ya Ushirika duniani kwa mwaka 2022 ambayo kitaifa yamefanyika Mkoani Tabora ,Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Said Pamui amesema pikipiki hizo zitakwenda kuwasaidia warajisi kuvitembelea vyama vya ushirika kwa urahisi katika maeneo yao pengine hata kwa mshirika mmoja mmoja.


Pamui amesema benki ya CRDB imekuwa na historia kubwa ya ushirika hivyo itahakikisha inaendelea kushirikiana na serikali ya awamu ya sita katika kuleta mageuzi makubwa ya kilimo tija kwa wakulima nchini.


Awali meneja wa biashara CRDB Kanda ya Magharibi Jumanne Wagana akimweleza Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe wakati alipotembelea banda la benki hiyo amesema mpaka sasa benki ya CRDB imetoa kiasi cha shilingi bilioni  494 katika kuinyanyua sekta ya kilimo.

Hata hivyo amesema benki ya CRDB imepunguza kiwango cha riba kwa wakulima kupitia kilimo kutoka 20% mpaka kufikia 9%.


Waziri Bashe ameipongeza benki hiyo huku akibainisha kuwa ni mwanzo mzuri kwa taasisi za kifedha kuanza kuwapa thamani wakulima.

Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Said Pamui (kulia) akizungumza wakati akimkabidhi Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe pikipiki nane (8) zenye thamani ya shilingi Milioni 24 .5 zitakazo kwenda kutumiwa na warajisi kama nyenzo ya usafiri.
Muonekano wa pikipiki nane (8) zenye thamani ya shilingi Milioni 24 .5 zilizotolewa na Benki ya CRDB kwa ajili ya warajisi kama nyenzo ya usafiri.

Muonekano wa pikipiki nane (8) zenye thamani ya shilingi Milioni 24 .5 zilizotolewa na Benki ya CRDB kwa ajili ya warajisi kama nyenzo ya usafiri.

Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe akisaini kitabu katika Banda la Benki ya CRBD

Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe akizungumza katika Banda la Benki ya CRBD


Post a Comment

0 Comments