Ticker

6/recent/ticker-posts

WCF YATOA ELIMU YA FIDIA KWA WAFANYAKAZI KWA MAAFISA UTUMISHI NA UTAWALA KUTOKA TAASISI ZA UMMA

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Morogoro

MFUKO wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF) umezidi kupanua wigo wa kufikisha elimu ya Fidia kwa Wadau wake ambapo safari hii walengwa wamekuwa Maafisa Utumishi na Utawala kutoka Taasisi na Mashirika ya Umma.

Maafisa hao wamejifunza masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na Elimu kuhusu Mafao ya Fidia kwa Wafanyakazi, Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi, lakini pia masuala ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi, kisha kujadiliana katika makundi.

Mafunzo hayo ya siku mbili yamefanyika mkoani Morogoro na yalifunguliwa Juni 13, 2022 na Mkurugenzi wa Huduma za Tathmini Dkt. Abdulsalaam Omar kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo.

“Hili ni kundi la kwanza la Maafisa Utumishi au Maafisa Utawala au Maafisa Rasilimali Watu kutoka katika taasisi za Umma kuja kupata mafunzo haya.” Alisema Dkt. Omar.

Alisema elimu kama hiyo ilianza kutolewa kwa Maafisa Utumishi kutoka katika Halmashauri ambapo hadi kufikia sasa Maafisa Utumishi na Utawala ambao tayari wamepatiwa mafunzo idadi yao inafikia 182.

“Kusudio letu tupate Maafisa Utumishi wengine takriban 100 kutoka katika taasisi za Umma.” Alifafanua.

Alisema Mfuko umekuwa ukitoa elimu kwa wadau mbalimbali wanaosaidia katika mchakato wa kutoa Fidia stahiki na kwa wakati kwa mfanyakazi aliyeumia, kuugua ama kufariki kutokana na kazi kwa mujibu wa mkataba.

“Mfuko wa Fidia umebaini kuwa maafisa utumishi na maafisa utawala ni kiungo muhimu katika kazi zetu sisi kama Mfuko, kwa sababu hawa wafanyakazi wanapopata changamoto hatua ya kwanza wanawataarifu ninyi na nyiekwa mujibu wa sharia ndio wenye wajibu wa kumtaarifu Mkurugenzi Mkuu kwa niaba ya waajiri wenu, hivyo tumeona ni muhimu kwenu kupata elimu hii.” Alisisitiza.

Kwa upande wao washiriki wamefurahishwa na elimu waliyoipata kwani kupitia mafunzo hayo kila mmoja ataenda kutenda kwa usahihi kwa mujibu wa sharia na miongozo.

“Huduma ya Mtandao ninaamini ni kitu kizuri sana kwa sisi waajiri kwani tunaweza kuingia kwenye mtandao na kutoa taarifa kwa wakati ili mtumishi aweze kupata syahiki yake kwa wakati.” Alisema Bi. Leila Komba, Afisa Utumishi Mwandamizi Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Aidha Wameushukuru Mfuko kwa kutoa mafunzo hayo na wangetamani yawe endelevu.

“Sisi tuliobahatika kupata mafunzo haya basi tukawafundishe wenzetu wakiwemo waajiri wetu.” Alisema mshiriki mwingine Bi. Leticia Machibya kutoka Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

Akifunga mafunzo hayo leo Juni 14, 2022, Afisa Tawala Msaidizi anayeshughulikia Rasilimali Watu Mkoa wa Morogoro, Bw. Herman Tesha ametoa rai kwa washiriki kuitumia elimu waliyoipata kuwasaidia wafanyakazi sehemu wanakotoka kuweza kupata stahiki zao pindi wanapokumbwa na changamoto za kuumia, kuugua au kufariki kutokana na kazi.

“Mtakuwa mmepata mambo mengi mapya ambayo hamkuwa nayo hapo awali, mimi binafsi nimeshawahi kuhudhuria mafunzo kama haya na nimefaidika sana, nitoe rai kwenu nyote mtumie elimu mliyoipata ili kuwasaidia wafanyakazi wenu kupata stahiki zao pindi wanapoumia, kuugua ama kufariki kutokana na kazi, na kwa kufanya hivyo mtakuwa mmeusaidia Mfuko kutimiza lengo la kuanzishwa kwake. ” Alisisitiza na kutoa mfano… mimi mwenyewe ofisini kwangu, watumishi wetu watatu walifaidika na Mfuko huu mmoja alifariki na wategemezi wake wanaendelea kufaidika,” Alisema.


Mkurugenzi wa Huduma za Tathmini Dkt. Abdulsalaam Omar, akitoa Mada kuhusu Mafao yanayotolewa na Mfuko


Mkurugenzi wa Huduma za Tathmini Dkt. Abdulsalaam Omar, akizungumza na Maafisa Utumishi na Maafia Utawala kutoka taasisi za Umma.


Baadhi ya Maafisa Utumishi na Maafia Utawala kutoka taasisi za Umma, wakiwa kwenye mafunzo hayo.


Meneja Tathmini za Vihatarishi Sehemu za Kazi, Bi. Naanjela Msangi, akitoa mada kuhusu usalama na afya mahali pa kazi.





Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Elimu kwa Umma, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bi. Laura Kunenge akizungumza na washiriki


Afisa Tathmini za Vihatarishi Sehemu za Kazi WCF, Bw. Robert Duguza, akifuatilia mijadala kwenye makundi.



Afisa Mfawidhi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Mkoani Morogoro, Bw. Athumani Khalfan, akitoa mada kuhusu Sheria ya Fidia.


Katibu Tawala Msaidizi anayeshughulikia masuala ya Rasilimali Watu na Utawala Mkoa wa Morogoro Bw.

Mshiriki wa mafunzo, Bi. Leticia Machibya, akizungumza kwa niaba ya wenzake.



Mshiriki akionyesha jinsi alivyoweza kupata ukurasa wenye maelekezo ya kutoa taarifa kwa njia ya mtandao kupitia WCF Portal


Bi. Tumaini Kyando kutoka WCF, akifuatilia mjadala kwenye makundi


Majadiliano ya vikundi.

Post a Comment

0 Comments