Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akifungua Mkutano na wahariri wa Vyombo vya Habari Nchini. Mkutano huo umefanyika leo Juni 4,2022 Jijini Dar es Salaam.Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza kwenye Mkutano na wahariri wa Vyombo vya Habari Nchini. Mkutano huo umefanyika leo Juni 4,2022 Jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Allan Kijazi akizungumza kwenye Mkutano na wahariri wa Vyombo vya Habari Nchini. Mkutano huo umefanyika leo Juni 4,2022 Jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri nchini (TEF), Deodatus Balile akizungumza kwenye Mkutano wa Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi na wahariri wa Vyombo vya Habari Nchini. Mkutano huo umefanyika leo Juni 4,2022 Jijini Dar es Salaam. Baadhi ya wahariri wa Vyombo vya Habari Nchini wakifuatilia Mkutano na Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Mkutano huo umefanyika leo Juni 4,2022 Jijini Dar es Salaam.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
************************
WAZIRI Wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula amesema kuwa Mkoa wa Dar es Salaam umekithiri kwa uvamizi wa ardhi hasa kwa baadhi ya wananchi kununua maeneo na kuyaendeleza bila kujua uhalali wa umiliki wa eneo husika.
Waziri Mabula ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano ulioikutanisha Wizara hiyo na jukwaa wahariri wa vyombo vya habari nchini kupitia Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF.)
"Hali ya uvamizi wa ardhi kwa Mkoa wa Dar es Salaam imekithiri kwa kiasi kikubwa, watu wana hati za umiliki wa maeneo lakini hawataki kuendeleza maeneo hayo...Wanatokea wajanja wanauza eneo hilo kwa mtu mwingine ambaye haulizi uhalali wa eneo hilo kwa ofisi husika anajenga kumbe amevamia eneo la mtu...." Amesema.
Aidha amesema kuwa, ni vyema wananchi wakazitumia ofisini za ardhi zilizopo kote nchini wakitaka kujenga au kuendeleza maeneo kabla ya kukumbana na kadhia ya uvamizi pindi sheria inapofuata mkondo wake.
"Wananchi wasifikiri wakivamia maeneo ya watu watarasimishiwa maeneo hayo, ukivamia eneo sheria ikafuata mkondo wake kilio kisirudi kwetu...nitoe rai, mjiridhishe kabla ya kufanya endelezaji wa maeneo hayo." Amesema Waziri Mabula.
Pia amesema kuwa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imetoa shilingi Bilioni 50 kwa Wizara hiyo ambazo zimeelekezwa kwa Halmashauri 55 katika mradi wa KKK (Kupanga, Kupima na Kumilikisha) kwa kasi maeneo, mradi huo unashirikisha Serikali na Taasisi binafsi katika kuhakikisha jamii pia inapata uelewa kuhusiana na umiliki wa ardhi na umuhimu wa upangaji wa miji.
" Tunashukuru Rais Samia kwa kutoa fedha zilizoelekezwa katika Halmashauri 55, baada ya Royal Tour nchi zote zinaitazama Tanzania Wizara imejipanga hatutamwangusha Rais katika kasi yake ya kuifungua nchi na tukiwa kiungo muhimu kwa nchi na uchumi katika uwekezaji, kilimo, mifugo na miundombinu tumetenga maeneo ya kutosha katika miji 27 tayari kwa kuwapokea wawekezaji...." Amesema.
Waziri Mabula amewataka wahariri na waandishi kutumia vyema kalamu zao kwa kuandika habari zenye tija kwa jamii na zisizoleta sitofahamu kwa jamii.
Awali Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Allan Kijazi amesema kikao hicho kimelenga kubadilishana mawazo na kujadili namna ya kutatua changamoto katika sekta hiyo muhimu, tegemeo na msingi wa uchumi wa maendeleo ya nchi.
Kijazi amesema vyombo vya habari vina mchango mkubwa hasa kwa kuwasemea wananchi na kuwapa mrejesho kutoka kwa Serikali juu ya nini kinafanyika na Wizara hiyo itaendelea kushirikiana na Vyombo vya habari katika kuhakikisha wananchi wanapata taarifa zote muhimu za Wizara hiyo.
0 Comments