Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. Lughano Kusiluka akizungumza na washiriki wa wa mafunzo ya siku tatu ya Chama cha Washauri wa Wanafunzi Tanzania (TACOGA1984) leo Juni 22, 2022, katika ukumbi wa mkutano wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Jijini Arusha.
Mwenyekiti wa Chama cha Washauri wa Wanafunzi Tanzania (TACOGA1984) Bi. Sophia Nchimbi akizungumza jambo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu ya Chama cha Washauri wa Wanafunzi Tanzania (TACOGA1984) leo Juni 22, 2022, katika ukumbi wa mkutano wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Jijini Arusha.
Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Mipango, Fedha na Utawala wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Dr. Shubi Kaijage akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu ya Chama cha Washauri wa Wanafunzi Tanzania (TACOGA1984) leo Juni 22, 2022, katika ukumbi wa mkutano wa Taasisi hiyo Jijini Arusha.
Washiriki wa Mafunzo ya Chama cha Washauri wa Wanafunzi Tanzania (TACOGA1984) wakimsikiliza mgeni rasmi ambaye ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof.Lugano Kusiluka (hayupo katika picha) wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu ya Chama hicho leo Juni 22, 2022, katika ukumbi wa mkutano wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Jijini Arusha.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. Lughano Kusiluka(katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Washauri wa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu na Kati baada ya kufungua mafunzo ya siku tatu ya Chama cha Washauri wa Wanafunzi Tanzania (TACOGA1984) leo Juni 22, 2022, katika ukumbi wa mkutano wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Jijini Arusha.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. Lughano Kusiluka (Katika Waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Serikali za Wanafunzi kutoka katika vyuo mbalimbali baada ya kufungua mafunzo ya siku tatu ya Chama cha Washauri wa Wanafunzi Tanzania (TACOGA1984) leo Juni 22, 2022, katika ukumbi wa mkutano wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Jijini Arusha
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. Lughano Kusiluka (Katikati Waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Chama cha Washauri wa Wanafunzi Tanzania(TACOGA 1984) baada ya kufungua mafunzo ya siku tatu ya Chama hicho leo Juni 22, 2022, katika ukumbi wa mkutano wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Jijini Arusha.
…………………………………..
Na Mwandishi Wetu.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. Lughano Kusiluka amezitaka Taasisi za Vyuo Vikuu na Vyuo vya Kati kuwawezesha Washauri wa Wanafunzi kuhudhuria mafunzo ya ushauri yanayoratibiwa na Chama cha Ushauri wa Wanafunzi Tanzania (TACOGA1984) ili kuwajengea uwezo katika utendaji wao.
Prof. Kusiluka amesema hayo leo Juni 22, 2022, wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu ya Chama cha Washauri wa Wanafunzi Tanzania (TACOGA 1984) katika ukumbi wa mkutano wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Jijini Arusha.
“Mafunzo haya ni muhimu kwetu sote siyo tu kwa wanafunzi bali Jamii yetu yote, kupitia mafunzo haya tunakuwa tumejenga Jamii bora kwa nchi yetu ” amesema Prof. Kusiluka
Aidha, ameongeza kuwa ni muhimu kwa washauri wa wanafunzi kuwa na mafunzo ya mara kwa mara ili waweze kutoa ushauri wenye kujenga na kuwapata wasomi bora wenye kutumikia taifa lao.
“wito wangu kwa wazazi tushirikiane kwa karibu na waalimu pamoja na washauri ili kuwalea wanafunzi katika mazingira mazuri yenye kuzingatia maadili mema” amesisitiza Prof. Kusiluka
Kwa upande wake Mwenyekiti wa TACOGA (1984) Bi. Sophia Nchimbi, ameeleza kuwa, lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo washauri wa wanafunzi waweze kufanya kazi zao kwa kufuata miongozo na kuwasaidia wanafunzi kuishi kwa kuzingatia maadili mema .
“Mada zitakazotolewa katika mafunzo haya ni 12 zikiwa na lengo la kuwajengea uwezo washauri wa wanafunzi katika masuala mbalilmabli ikiwemo namna ya kuandika maombi ya miradi, kuongea mbele ya hadhara na kuwashauri wanafunzi “ amesema Bi. Sophia Nchimbi
Naye mshiriki wa Mafunzo hayo ambaye ni Waziri Mkuu wa Serikali ya Wanafunzi kutoka Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni Ndg. Ajubi Ally ameeleza kuwa, mafunzo hayo yatamsaidia katika kuwaongoza na kuwashauri wanafunzi wenzake namna ya kuishi kwa kuzingatia maadili na kuondokana na hofu pale wanapokutana na changamoto mbalimbali vyuoni.
0 Comments