Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari , Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dk.Jimmy Yonazi (Mwenye Suti) akizungumza na Watendaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Uongozi wa Wilaya Handeni wakati wa ushushaji wa mnara kwa ajili ya huduma za mawasiliano katika kijiji cha Msomera wilayani Handeni mkoani mkoani Tanga kwa ajili wananchi waliohamishwa Ngongoro wakati Katibu wa Wizara hiyo alipotembelea Kijiji hicho kuangalia huduma za Mawasiliano.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari , Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dk.Jimmy Yonazi (Mwenye Suti) akizungumza na Watendaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Uongozi wa Wilaya Handeni wakati wa ushushaji wa mnara kwa ajili ya huduma za mawasiliano katika kijiji cha Msomera wilayani Handeni mkoani mkoani Tanga kwa ajili wananchi waliohamishwa Ngongoro wakati Katibu wa Wizara hiyo alipotembelea Kijiji hicho kuangalia huduma za Mawasiliano.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dk.Jabiri Bakari akiangalia mfumo wa maji katika kijiji cha Msomero wilayani Handeni mkoani Tanga kwa ajili ya wananchi wanaohamia kutoka Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro kwa kuanza makazi wakiwa na huduma mbalimbali.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari , Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dk.Jimmy Yonazi (Mwenye Suti) akipata maelezo kutoka Mkuu wa Kanda ya Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi Imelda Salum (alionyoosha mkono) wakati wa ushushaji wa mnara muda wa kampuni ya Airtel kwa ajili ya huduma za mawasiliano katika kijiji cha Msomero wilayani Handeni mkoani mkoani Tanga kwa ajili wananchi waliohamishwa Ngongoro wakati Katibu wa Wizara hiyo alipotembelea Kijiji hicho kuangalia huduma za Mawasiliano.
***************************
Na Mwandishi Wetu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Dkt. Jimmy Yonazi amewahakikishia wakazi wa kijiji cha Msomero wilayani Handeni mkoani Tanga na wageni watakaohamia kutokea Ngorongoro uhakika wa kupata huduma bora za mawasiliano wawapo Msomero.
Akizungumza katika ziara ya kukagua upatikanaji wa huduma za mawasiliano katika kijiji cha Msomero leo Dkt. Yonazi amesema serikali inatambua umuhinu wa mawasiliano katika kukuza uchumi hivyo wizara pamoja na taasisi zilizo chini yake wamejipanga kuhakikisha mawasiliano hayayumbi.
Dkt Yonazi ameiagiza Mamlaka ya Mawasiliano TCRA kuhakikisha kuwa inawaelekeza watoa huduma wote wa mawasiliano kwenda kuwekeza na kutoa huduma za mawasiliano kijiji huko ili watumiaji wapate wigo mpana zaidi wa kuchagua.
Akizumgumza katika ziara hiyo Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano TCRA Dkt Jabir Bakari amesema TCRA itatekeleza agizo hilo mara moja na kuongeza kuwa katika kuitikia wito wa kuboresha mawasiliano TCRA ili kuweza kurahisisha huduma ndani ya kijiji na kuweza kufanya biashara kwa kutumia mtandao.
Nae Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (USCAF) Justina Mashiba amesema mfuko wao utafadhili maabara ya TEHAMA katika shule ya Msingi ikiwa ni hatua ya kuwajengea msingi wa TEHAMA kuanzia wakiwa wadogo.
Akizungumzia maendeleo ya matayarisho ya kijiji cha Msomero kupokea wageni kutoka Ngorongoro Mkuu wa wilaya ya Handeni Mhe. Siriel Mchembe amesema Kijiji cha Msomero kiko tayari kupokea wageni ambapo huduma zote za msingi ikiwepo makazi, maji, umeme, shule, majosho na maji kwa ajili ya mifugo yako tayari.
0 Comments