Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda akizungumza kwenye hafla ya utiaji saini mkataba wa mradi wa elimu ya juu kwa ajili ya mageuzi ya kiuchumi kati ya taasisi za elimu ya juu HEET PROJECT na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia kutoka Benki ya Dunia wenye thamani ya shilingi Bilioni 972. Hafla hiyo imefanyika leo Juni 19,2022 Jijini Dar es salaam Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Mhe.Omary Kipanga akizungumza kwenye hafla ya utiaji saini mkataba wa mradi wa elimu ya juu kwa ajili ya mageuzi ya kiuchumi kati ya taasisi za elimu ya juu HEET PROJECT na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia kutoka Benki ya Dunia wenye thamani ya shilingi Bilioni 972. Hafla hiyo imefanyika leo Juni 19,2022 Jijini Dar es salaam Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt.Francis Michael akizungumza kwenye hafla ya utiaji saini mkataba wa mradi wa elimu ya juu kwa ajili ya mageuzi ya kiuchumi kati ya taasisi za elimu ya juu HEET PROJECT na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia kutoka Benki ya Dunia wenye thamani ya shilingi Bilioni 972. Hafla hiyo imefanyika leo Juni 19,2022 Jijini Dar es salaam Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. James Mdoe akizungumza kwenye hafla ya utiaji saini mkataba wa mradi wa elimu ya juu kwa ajili ya mageuzi ya kiuchumi kati ya taasisi za elimu ya juu HEET PROJECT na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia kutoka Benki ya Dunia wenye thamani ya shilingi Bilioni 972. Hafla hiyo imefanyika leo Juni 19,2022 Jijini Dar es salaam Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Caroline Nombo, akizungumza kwenye hafla ya utiaji saini mkataba wa mradi wa elimu ya juu kwa ajili ya mageuzi ya kiuchumi kati ya taasisi za elimu ya juu HEET PROJECT na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia kutoka Benki ya Dunia wenye thamani ya shilingi Bilioni 972. Hafla hiyo imefanyika leo Juni 19,2022 Jijini Dar es salaam
Mkuu wa Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE), Prof.Stephen Maluka akiwa kwenye hafla ya utiaji saini mkataba wa mradi wa elimu ya juu kwa ajili ya mageuzi ya kiuchumi kati ya taasisi za elimu ya juu HEET PROJECT na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia kutoka Benki ya Dunia wenye thamani ya shilingi Bilioni 972. Hafla hiyo imefanyika leo Juni 19,2022 Jijini Dar es salaam. Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof.William Anangisye akiwa kwenye hafla ya utiaji saini mkataba wa mradi wa elimu ya juu kwa ajili ya mageuzi ya kiuchumi kati ya taasisi za elimu ya juu HEET PROJECT na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia kutoka Benki ya Dunia wenye thamani ya shilingi Bilioni 972. Hafla hiyo imefanyika leo Juni 19,2022 Jijini Dar es salaam
Baadhi ya wakuu wa Vyuo na Taasisi za Elimu ya Juu wakiwa kwenye hafla ya utiaji saini mkataba wa mradi wa elimu ya juu kwa ajili ya mageuzi ya kiuchumi kati ya taasisi za elimu ya juu HEET PROJECT na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia kutoka Benki ya Dunia wenye thamani ya shilingi Bilioni 972. Hafla hiyo imefanyika leo Juni 19,2022 Jijini Dar es salaam Baadhi ya wakuu wa Taasisi za Elimu wakisaini mkataba wa mradi wa elimu ya juu kwa ajili ya mageuzi ya kiuchumi kati ya taasisi za elimu ya juu HEET PROJECT na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia kutoka Benki ya Dunia wenye thamani ya shilingi Bilioni 972.Hafla hiyo imefanyika leo Juni 19,2022 Jijini Dar es salaam
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
**************************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amewataka wakuu wa vyuo kusimamia fedha za utekelezaji wa mradi wa elimu ya juu kwa ajili ya mageuzi ya kiuchumi kati ya taasisi za elimu ya juu HEET PROJECT vizuri ili ziweze kutekeleza malengo yaliyokusudiwa.
Ameyasema hayo leo Waziri Mkenda wakati wa utiaji saini mkataba wa mradi wa elimu ya juu kwa ajili ya mageuzi ya kiuchumi kati ya taasisi za elimu ya juu HEET PROJECT na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia kutoka Benki ya Dunia wenye thamani ya shilingi Bilioni 972.
Amesema kutakua na mikoa 14 mipya ambapo vyuo vitafungua campus aidha wahiyari kwa kuwa wabunifu na ujuzi ili kuleta miradi ya elimu yenye tija kimataifa.
Aidha amevitaka vyuo kuwapeleka wahadhiri wake kwenda kimataifa zaidi kusoma na kufungua milango ya wahadhiri wa nje kuja kujifunza pia.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Mhe.Omary Kipanga amesema Wizara haitasita kuondoa fedha za utekelezaji wa miradi kwa taasisi yoyote iliyoko chini yake ambayo itachelewesha utekelezaji wa mradi wa Elimu ya juu kwa ajili ya mageuzi ya kiuchumi.
Aidha amesema mradi huo utatekelezwa katika Mikoa 16 huku Wanufaika wa mradi huo wa wakiwa ni Vyuo Vikuu 14,Taasisi tatu kutoka Wizara ya Elimu, Vyuo Vikuu vitano vilivyoko chini ya Wizara ya fedha hii ikiweka idadi ya wanufaika 23.
Nae Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe amesema Utekelezaji wa miradi hiyo iwe ya viwango kwa kadri ya maelekezo ya benki ya Dunia na serikali ya Tanzania na waratibu wa miradi wawe na ukaribu na watekelezaji wengine wa miradi ili kusiwe na kukwama katika utekelezaji.
"Kuna baadhi ya taasisi zinachukua muda mrefu kufanya utekelezaji wa miradi,lakini makubaliano katika mradi huu kama kutakuwepo na ucheleweshaji wa utekelezaji wa mradi Fedha zitachukuliwa na kipelekwa kwenye taasisi nyingine". Amesema Prof.Mdoe
0 Comments