**********************
Katika kuadhimisha kumbukukumbu Mtakatifu Antony wa Padua Wakristo ulimwenguni kote wamehimizwa kumtangaza kristo kwa watu wengine wanao wazunguka katika jamii ili kusudi watu hao wamjue kristo wamtambua pamoja na kumtumikia.
Wito huo Umetolewa na Padre Julius Lubuva Paroko wa Parokia ya Bikira Maria Mkingiwa Dhambi ya Asili-Haubi, Jimbo katoliki la Kondoa wakati wa Mahubili yake alie yatoa katika Misa Takatifu kwa waamini Kigango Cha Mtakatifu Anthony wa Padua-Chema, ambapo pia leo ni sherehe ya somo wa Jumuhiya kigangoni hapo.
Padre Lubuva amesema kuwa kila Mkristo awe nuru ya mkristo mwenzake katika kupeleka habari njema hasa kwa wale walio ludi nyuma katika Imani na wajisikie fahaja na kuwa na kifua mbele kumtukuza kristo wao.
Hata hivyo amewasihi wakristo kuendelea kujifunza na kuyaishi yale aliyo fundisha Mt. Antony wa Padua ikiwemo kuwahudumia watu kwa upendo pasipo kuwa na Ubaguzi wowote kwa kuwa watu wote ni sawa mbele ya Mungu.
Aidha Padre Lubuva amehitimisha Homilia yake kwa kuwata wakristo kuendelea kuwa tia moyo wale wanao pitia changamoto tofauti katika Imani kwa kufanya hivyo watakuwa nuru kwa watu wengine wanaowazunguka Katika kumtangaza kristo.
0 Comments