***************************
Mwenyekiti wa jumuiya ya umoja wa wanawake Tanzania (UWT) mkoa wa Njombe Bi,Scolastika Kevela ametoa wito kwa viongozi wanaotokana na Chama cha Mapinduzi kufanya kazi kwa bidii,juhudi na maarifa ili kumsaidia Rais pamoja na Chama katika utekelezaji wa Ilani ya Chama chao.
Bi,Kevela ametoa wito huo kwa viongozi mbali mbali wakiwemo Madiwani pamoja na wajumbe wa kamati ya utekelezaji wilaya ya Wanging’ombe alipofanya ziara ya kikazi katika wilaya hiyo.
“Tumsaidie sana Mh,Rais kumsaidia mheshimiwa Rais ni kufanya kazi kwa bidii mahali ulipo.Kama ni diwani wajibika kwa kipande chako,katibu kata wajibika kwa nafasi yako na ukiona umechukua nafasi halafu umekaa tu jua huitendei haki hiyo nafasi”alisema Bi,Kevela
Aidha ameongeza kuwa Rais Samia amekuwa akiendelea kufanya mambo makubwa katika sekta mbali mbali ikiwemo pia kuendelea kuitangaza nchi kimataifa hivyo ni muhimu sana kuendelea kumtia nguvu kwa kufanya kazi kwa ufasaha.
Evarista Kihombo na Paulina Samatta ni baadhi ya viongozi wanaotakana na jumuiya hiyo,wameshukuru mwenyekiti wao kwa kuendelea kuwakumbusha majukumu yao ya kiuongozi huku wakiahidi kuendelea kufanya kazi kwa juhudi ili kuijenga jumuiya na Chama.
“Kwa niaba ya madiwani wote pamoja na wajumbe,mimi napenda kukushukru sana mwenyekiti wa mkoa pamoja na katibu kwa ujio wenu na tunawahakikishia ukija tena siku nyingine kila kata itasema neno juu ya ujumbe wa leo”alisema Bi Samatta
Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Njombe Bi,Scolastika Kevela amefanya ziara hiyo ya kikazi katika wilaya ya Wanging’ombe mara baada ya kukamilisha ziara wilayani Ludewa huku akitarajiwa kuendelea na katika jimbo la Makambako,Lupembe pamoja na wilaya ya Makete.
0 Comments