Ticker

6/recent/ticker-posts

USHIRIKI WA TANZANIA KATIKA MKUTANO MKUU WA MAENDELEO YA MAWASILIANO DUNIANI, (ITU-WTDC-2022) UNAOFANYIKA JIJINI KIGALI, RWANDA


Ujumbe wa Tanzania ukishiriki kwenye Mkutano Mkuu wa Maendeleo ya Mawasiliano Duniani, unaofanyika jijini Kigali, Rwanda; ukiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Jim Yonazi (wa kwanza kulia), akifuatiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Jabiri Bakari (katikati) na Mkurugenzi wa Masuala ya Kisekta wa TCRA Dkt. Emmanuel Manasseh. Mkutano huo mbali na ajenda nyingine unajadili na kuweka mipango ya Maendeleo katika Sekta ya Mawasiliano Duniani ukiongozwa na Kauli mbiu isemayo “Kuunganisha Wasiounganishwa ili Kufikia Maendeleo Endelevu." Picha Na: TCRA


Wataalam wa Mawasiliano wakiiwakilisha Tanzania kwenye Mkutano Mkuu wa Maendeleo ya Mawasiliano Duniani, (ITU-WTDC-2022) unaofanyika jijini Kigali, Rwanda. Kutoka kulia ni Mwanasheria wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari (WHMTH) Bi. Eunice Masigati, Mhandisi Mwandamizi (WHMTH) Bi. Edith Turuka (katikati) na Meneja wa Rasilimali za Mawasiliano na Teknolojia-TCRA Mhandisi Mwesigwa Felician. Mkutano huo unaozihusisha nchi wanachama wa Shirika la Mawasiliano Duniani (ITU) unajadili mikakati ya kukuza sekta mawasiliano na TEHAMA. Picha na: TCRA.


Sehemu ya washiriki wa Mkutano Mkuu wa Maendeleo ya Mawasiliano Duniani, (ITU-WTDC-2022) unaofanyika jijini Kigali, Rwanda, ukifanyika kwa mara ya kwanza barani Afrika. Tanzania inawakilishwa kwenye Mkutano huo na Ujumbe kutoka Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari (WHMTH) na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania -TCRA. ITU-WTDC-2022 unazileta pamoja nchi wanachama wa Shirika la Mawasiliano Duniani (ITU) kujadili mikakati ya kukuza sekta mawasiliano na TEHAMA ukifanyika kama mkutano wa maandalizi kuelekea Mkutano Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Duniani – ITU-PP. ITU-PP ni Kongamano lenye nguvu ya maamuzi katika Shirika la Mawasiliano la Umoja wa Mataifa; pia ni chombo cha kuunda na kuridhia mikataba mbalimbali ya mawasiliano kimataifa ambapo hujadili muelekeo wa teknolojia za mawasiliano kimataifa. ITU-PP kinaundwa na nchi zote 193 wanachama wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mawasiliano na hukutana kila baada ya miaka minne, ambapo mwaka huu 2022 Tanzania inawania Ujumbe wa Baraza la ITU katika Mkutano utakaofanyika jijini Bucharest, Romania baadae mwezi Septemba, 2022. Picha na: TCRA

Post a Comment

0 Comments