Ticker

6/recent/ticker-posts

TBS,FCC WAONYA WAZALISHAJI WA BIDHAA BANDIA


Mkurugenzi Mkuu wa TBS Dkt.Athuman Ngenya(Kulia)na Mkurugenzi Mkuu wa FCC Bw. William Erio(kushoto)wakionesh tofauti kati ya bidhaa feki na halisi ya vifaa vya umeme. TBS na FCC wametoa wito kwa wananchi kupiga vita bidhaa hafifu na bandia kwani zina madhara ya kiafya na uchumi.Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS)Dkt.Athuman Yusuf Ngenya akitoa wito kwa wafanyabiashara wanaoingiza bidhaa nchini hususani vifaa vya umeme kuhakikisha wanazingatia ubora, katika mkutano kati ya waandishi wa habari TBS na FCC mapema leo.Mkurugenzi Mkuu wa FCC Bw. William Erio(kushoto) akitoa wito kwa wafanyabiashara wanaoingiza bidhaa nchini hususani vifaa vya umeme kuhakikisha wanazingatia ubora, katika mkutano kati ya waandishi wa habari TBS na FCC mapema leo.

*******************

Shirika la Viwango Tanzania (TBS ) na Tume ya Ushindani FCC wamesema mfanyabiashara yeyote atakayekutwa na bidhaa bandia sokoni, atachukuliwa hatua za kisheria ikiwepo kufutiwa leseni, kutozwa faini pamoja na kufikishwa Mahakamani.

TBS na FCC wamesema baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu wamekuwa wakidurufu nembo za bidhaa halisi na kuziweka kwenye bidhaa bandia na kuziingiza sokoni hali inayotishia usalama wa afya za watumiaji wa bidhaa hizo. Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa TBS Dkt.Athuman Ngenya amesema hatua za kisheria zitafuatwa ikiwepo kufutiwa leseni. “Imebainika kwamba kuna wimbi kubwa la wafanyabiashara wasio waaminifu, wanaingiza sokoni bidhaa zisizo na viwango kwa mgongo wa bidhaa ambazo zinakidhi viwango, kwa mfano imegundulika hivi karibuni kwamba wanatanguliza kwenye makontena bidhaa halisi, kwa mfano wanatanguliza kontena moja ambalo lina bidhaa zinazokidhi viwango, lakini makontena yote yanayobaki ni bandia matokeo yake mnunuaji ananunua bidhaa akifikiri ni halisi, sasa tumeonelea ni vyema kuanza kutoa elimu na baadae kuanza kuchukua hatua za kisheria” amesema Dkt Ngenya. Kwa Upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani FCC Bw. William Erio amesema kuhusika kwa kuuza au kuzalisha bidhaa bandia ni kosa na hivyo kuwataka wafanyabiashara kuacha mara moja na badala yake wafuate sheria ikiwemo kuzisajili au kuthibitisha ubora wa bidhaa zao. “Nitumie fursa hii pia kutoa onyo kwa wazalishaji watambue, kwanza kujishughulisha na bidhaa bandia ni kosa la jinai kwa mujibu wa sheria za nchi yetu, wewe ikiwa unaingiza, unahifadhi, unasambaza, unanunua, ujue kwamba ukikutwa unafanya hivyo kuna faini kati ya shilingi Milioni 10 hadi 50, au mara tatu ya thamani ya bidhaa uliyokamatwa nayo na ile bidhaa tunaiteketeza, lakini pia unaweza kupata kifungo cha kati ya miaka mitano hadi kumi na tano, niwasihi watu wote waache” amesema Bw. Erio.

Post a Comment

0 Comments