Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi yaendayo kwa haraka (DART), Dkt.Edwin Muhede akiwa pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) Bi.Latifa Khamisi wakisaini mkataba wa makubaliano katika urahisishaji wa usafiri wa mabasi yaendayo haraka kipindii cha Maonesho ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba ya mwaka 2022. Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi yaendayo kwa haraka (DART), Dkt.Edwin Muhede akiwa pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) Bi.Latifa Khamisi wakibadilishana mikataba mara baada ya kusaini mkataba wa makubaliano katika urahisishaji wa usafiri wa mabasi yaendayo haraka kipindii cha Maonesho ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba ya mwaka 2022.Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi yaendayo kwa haraka (DART), Dkt.Edwin Muhede akiwa pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) Bi.Latifa Khamisi wakionesha mikataba waliosaini katika urahisishaji wa usafiri wa mabasi yaendayo haraka kipindii cha Maonesho ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba ya mwaka 2022.Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi yaendayo kwa haraka (DART), Dkt.Edwin Muhede akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika ofisi za Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) leo Juni 6,2022. Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi yaendayo kwa haraka (DART), Dkt.Edwin Muhede akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya utiaji saini wa makubaliano kati ya TANTRADE na DART katika urahisishaji wa usafiri wa mabasi yaendayo haraka kipindii cha Maonesho ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba ya mwaka 2022.Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi yaendayo kwa haraka (DART), Dkt.Edwin Muhede akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya utiaji saini wa makubaliano kati ya TANTRADE na DART katika urahisishajiwa usafiri wa mabasi yaendayo haraka kipindii cha Maonesho ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba ya mwaka 2022. Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) Bi.Latifa Khamisi akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya utiaji saini wa makubaliano kati ya TANTRADE na DART katika urahisishaji wa usafiri wa mabasi yaendayo haraka kipindii cha Maonesho ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba ya mwaka 2022.Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) Bi.Latifa Khamisi akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya utiaji saini wa makubaliano kati ya TANTRADE na DART katika urahisishaji wa usafiri wa mabasi yaendayo haraka kipindii cha Maonesho ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba ya mwaka 2022.Afisa Sheria Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) Bi.Emma Msofe akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya utiaji saini wa makubaliano kati ya TANTRADE na DART katika urahisishaji wa usafiri wa mabasi yaendayo haraka kipindii cha Maonesho ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba ya mwaka 2022.Mwanasheria wa Wakala wa Mabasi yaendayo kwa haraka (DART ), Bi.Domina Madeli akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya utiaji saini wa makubaliano kati ya TANTRADE na DART katika urahisishaji wa usafiri wa mabasi yaendayo haraka kipindii cha Maonesho ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba ya mwaka 2022. Kaimu meneja wa Mipango ya Usafirishaji DART Bw.Mohamed Kuganda akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya utiaji saini wa makubaliano kati ya TANTRADE na DART katika urahisishaji wa usafiri wa mabasi yaendayo haraka kipindii cha Maonesho ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba ya mwaka 2022. Meneja Masoko wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) Bi.Grace Lemunge akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya utiaji saini wa makubaliano kati ya TANTRADE na DART katika urahisishaji wa usafiri wa mabasi yaendayo haraka kipindi cha Maonesho ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba ya mwaka 2022.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
**************************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) wameingia makubaliano na Wakala wa Mabasi yaendayo kwa haraka (DART) katika utumiaji wa magari yaendayo haraka kurahisha usafirishaji wa wananchi ambao watakaoshiriki Maonesho ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba ya mwaka 2022.
Akizungumza na waandishi wa habari katika hafla hiyo iliyofanyika katika Ofisi za TANTRADE leo Juni 6,2022 Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) Bi.Latifa Khamisi amesema katika mpango huo mfupi lengo ni kuhakikisha kunakuwa na huduma za usafiri kirahisi kwa washiriki na watembeleaji wa maonesho ya sabasaba.
Amesema wamekuwa wakijitahidi kuhakikisha wanaleta kitu kipya kila mwaka wa Maonesho ya Sabasaba hivyo kwa mwaka huu wameamua kuleta suala la urahisishaji wa usafiri kwa washiriki wa Maonesho hayo.
"Washiriki wa Maonesho wataweza kuchukuliwa kutoka kituo cha Gerezani moja kwa moja na kuletwa hapa katika Maonesho ya Sabasaba, tunataka wananchi watambue kuna urahisi wa kufika na kuondoka hapa kupitia mabasi ya DART". Amesema Bi.Latifa.
Nae Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi yaendayo kwa haraka (DART), Dkt.Edwin Muhede amesema kutakuwa na maegesho ya magari katika ameneo maalumu waliyoyaandaa ili kuondokana na msongamano wa magari kwenye sehemu moja na mengine kukosa sehemu ya kuegesha.
Amesema tiketi za kuingia katika viwanja vya maonesho zitakuwa zinapatikana pia katika vituo maalumu vya Mabasi yaendayo kwa haraka ili kuondokana na usumbufu wa kupanga foleni kusubiri tiketi katika maeneo ya Maonesho.
aidha amesema ukichana na suala la usafiri kwenye maonesho hayo DART kwa kushirikiana na wadau wao wamepanga kuleta huduma ya bure ya internet (Free Public Wife) katika Maonesho hayo yatakapoanza hivi karibuni.
"Hili ni jambo la kwanza na tunajivunia katika ushirikiano huu na TANTRADE na ninaamini litaenda kuleta matokeo makubwa kwa wadau wetu, hivyo wafanyabiashara wote mnakaribishwa na kutumia huduma hii kujitangaza". Amesema Dkt.Muhede.
0 Comments