*************************
Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' imekubali kichapo cha mabao 2-0 dhidi ya Algeria katika Uwanja wa Benjamin Mkapa na kusalia nafasi ya 3 katika kundi F ikiwa na pointi 1.
Nafasi ya nne yupo Uganda akiwa na pointi 1 na Algeria anaongoza kundi akiwa na alama 6 baada ya kushinda mechi mbili huku Niger akiwa nafasi ya pili na alama 2.
Mechi ijayo Stars itacheza dhidi ya Uganda Septemba 19 ugenini kisha kurudiana Septemba 27 kwa Mkapa.
0 Comments