Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akikata utepe kuzindua rasmi Vitendea kazi vya uendelezaji wa kilimo katika Mashamba ya Miwa yaliyopo kwenye Kiwanda cha Sukari cha Kagera Sugar Mkoani Kagera tarehe 09 Juni, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kiwanda cha Sukari cha Kagera Sugar Bw. Seif Ali Seif mara baada ya kuzindua rasmi Vitendea kazi vya uendelezaji wa kilimo katika Mashamba ya Miwa yaliyopo kwenye Kiwanda cha Sukari cha Kagera Sugar tarehe 09 Juni, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Wafanyakazi wa Kiwanda cha Kagera Sugar wakati alipotembelea kiwanda hicho kilichopo Mkoani Kagera tarehe 09 Juni, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi Udege kuhusu uandaaji na uchakataji wa Miwa wakati alipotembelea kiwanda cha Kagera Sugar kilichopo Mkoani Kagera tarehe 09 Juni, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipata maelezo kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanroad Mhandisi Rogatus Mativila kuhusu kukamilika kwa Daraja la Kitengule linalounganisha Wilaya ya Misenyi na Karagwe Mkoani Kagera tarehe 09 Juni, 2022. Mhe. Rais Samia anaendelea na ziara yake ya siku ya pili Mkoani Kagera kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya Maendeleo ya Wananchi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiondoa kitambaa kuzindua rasmi Mtambo wa kuzalisha Umeme Megawati 20 katika Kiwanda Kagera Sugar Mkoani Kagera tarehe 09 Juni, 2022. Mhe. Rais Samia anaendelea na ziara yake ambayo ni siku ya pili Mkoani Kagera kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya Maendeleo ya Wananchi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akikata utepe kuzindua rasmi Mtambo wa kuzalisha Umeme Megawati 20 katika Kiwanda cha Kagera Sugar Mkoani Kagera tarehe 09 Juni, 2022. Mhe. Rais Samia anaendelea na ziara yake Mkoani humo kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya Maendeleo ya Wananchi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akitembelea Kiwanda cha Kagera Sugar Mkoani Kagera tarehe 09 Juni, 2022. Mhe. Rais Samia anaendelea na ziara yake ambayo ni siku ya pili Mkoani humo kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya Maendeleo ya Wananchi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Viongozi na Wananchi pamoja na Wafanyakazi wa Kiwanda cha Sukari cha Kagera Sugar mara baada ya kutembelea kiwanda hicho kilichopo Mkoani Kagera tarehe 09 Juni, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Kiwanda cha Kagera Sugar, mara baada ya kutembelea kiwanda hicho kilichopo Mkoani Kagera tarehe 09 Juni, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizindua Mradi wa Maji Kyaka- Bunazi Wilayani Misenyi Mkoani Kagera tarehe 09 Juni, 2022. Mhe. Rais Samia anaendelea na ziara yake ya siku tatu Mkoani Kagera kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya Maendeleo ya Wananchi. wa pili kulia ni Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso.
********************
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka wawekezaji katika viwanda vya sukari nchini kuchangia kikamilifu kufanikisha malengo ya kujitosheleza.
Rais Samia amesema hayo leo alipotembelea kiwanda cha Sukari cha Kagera Sugar kilichopo Missenyi mkoani humo na kutaka tufikie ziada ya kuuza nchi za nje ifikapo 2025.
Aidha, Rais Samia amesema Serikali imeazimia kufanya mageuzi ya kilimo cha kisasa ambayo yanapaswa kwenda sambamba na mahitaji ya viwanda vya ndani ili kuifanya nchi iweze kuwa mzalishaji mkubwa wa mazao ya kilimo Afrika.
Katika kutekeleza mageuzi hayo, Rais Samia amesema Serikali imetenga shilingi bilioni 20 kwa ajili ya kuanzisha kilimo cha alizeti na michikichi mkoani humo.
Rais Samia amesema lengo la kuanzisha kilimo cha mazao hayo ni kuzalisha mafuta ya kujitosheleza ndani ya nchi, kuwawezesha vijana kujiajiri na kuinua uchumi wa Mkoa huo.
Vile vile, Rais Samia amewataka wawekezaji kuiga mfano wa Mwekezaji wa kiwanda cha Kagera Sugar kwa kuajiri vijana katika shughuli muhimu za kilimo ambao wengi wao ni wahitimu wa vyuo mbalimbali vya hapa nchini.
Aidha, Rais Samia amewahakikishia wawekezaji kuwa Serikali itaendelea kuwawekea mazingira mazuri ya uwekezaji kwa kurekebisha Sera, Sheria na Kanuni zitakazochochea uwekezaji endelevu.
0 Comments