*********************
Naibu waziri wa Afya, Mhe.Dkt Godwin Mollel, amewaagiza watumishi wa Afya mkoani ARUSHA kutoa huduma bora kwa wagonjwa kwa kuzingatia kanuni na maadili ya kazi yao.
Dkt Mollel, ametoa wito huo Jijini Arusha jana tarehe 13/6/2022 wakati akizungumza na watumishi wa afya katika hospitali ya SelianI , Mount Meru na Arusha Lutheran Medical Center mara baada ya kufanya ziara ya kikazi ambapo amesema kuwa wanapaswa kutoa huduma nzuri kwani ni lengo la seikali kuhakikisha wananchi wote wanafaidika.
“Mtoe huduma bora kwa kuafata kanuni na taratibu za afya kwa watu wote wanaokuja katika hospitali zenu” alisema Dkt. Molel.
Pia kutokana na kipindi cha msimu mkubwa watalii katika jiji la Arusha, Dkt. Molel amewaomba wahudumu katika sekta ya Afya kushiriki kikalamilifu katika kuwahudumia watalii pindi wanapo fika kupata huduma za za Afya.
Ameeleza kuwa sekta ya Afya ni katika ya sekta ya muhimu katika utalii nchini hivyo kwamba Serikali kwa kutambua hilo imeanza mikakati mikubwa ikiwa ni pamoja na kuimarisha utoaji wa huduma za afya.
0 Comments