Ticker

6/recent/ticker-posts

MKUU WA MKOA WA RUVUMA AZINDUA TAMASHA LA MAJIMAJI SELEBUKA 2022

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Mh Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge, ameagiza ushiriki wa wilaya na halmashauri zote za Mkoa Wa Ruvuma kwenye tamasha la Majimaji Selebuka litakalofanyika kuanzia tarehe 23 hadi 30 July 2022 mjini Songea. Tamasha hili limekua jukwaa kuu la biashara, kutangaza utalii, kuchochea vipaji, utamaduni , mashindano ya debate kwa shule na michezo, hivyo linatoa fursa adimu kwa mkoa wetu wa Ruvuma.

Pia mwaka huu tamasha hili litakuwa na mashindano ya baiskeli ya km 165 toka Songea hadi Mbamba bay, mbio na mpira wa miguu na kikapu. Ili kuwapa urahisi washiriki kwenye Majimaji Selebuka imezindua tovuti yenye zaidi ya hoteli 200 kwa ajili wageni.

Pamoja na kutangaza vivutio vya utalii vya mkoa wa Ruvuma, Majimaji Selebuka inachochea biashara, elimu, sanaa, michezo kwenye ukanda wa kusini


Majimaji Selebuka ni tukio linalofanyika kila mwaka Songea, Ruvuma ambapo mwaka huu litazizima kuanzia tarehe 23 hadi 30 Julai. Kujisajili ingia majimajiselebuka.co.tz


Post a Comment

0 Comments