Na Mwandishi Wetu / Zanzibar
Kamati-tendaji ya Umoja wa Mawasiliano Afrika Mashariki (EACO) imejipambanua kukuza sekta ya mawasiliano Afrika Mashariki; mkakati uliowekwa bayana kwenye kikao-kazi cha Kamati hiyo kilichoketi, Bububu, Zanzibar mapema juma hili.
Kikao-kazi cha Kamati hiyo inayoundwa na Watendaji Wakuu wa Mamlaka za Usimamizi wa mawasiliano za Afrika Mashariki kilihudhuriwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano -Tanzania, Dkt. Jabiri Bakari, Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano-Kenya, Ezra Chiloba; Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Serikali wa Usimamizi wa Mawasiliano-Burundi, Samuel Muhizi; Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Sudani Kusini, Napoleon Adok Gai; Mkurugenzi Mkuu wa Kamisheni ya Mawasiliano -Uganda, Irene Kaggwa Sewankambo; Mtendaji Mkuu wa EACO Mtanzania Dkt. Ally Simba; na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano-Rwanda, Deo Muvunyi.
Akizungumza pembezoni mwa kikao hicho mtendaji mkuu wa EACO alisema “…tumedhamiria kuhakikisha mashirikiano baina ya taasisi zetu yanaimarika ili tukuze usimamizi thabiti wa huduma za mawasiliano katika nchi wanachama…” alisisitiza Simba.
EACO ulianzishwa mwaka 2012, kama muungano wa kikanda wenye sura ya kimataifa na kikanda ukilenga kuwaleta pamoja wasimamizi wa mawasiliano na wadau wa sekta ya mawasiliano Afrika Mashariki kwa shabaha ya kuboresha usimamizi na utoaji huduma za mawasiliano kwa wananchi wa Afrika Mashariki.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Jabiri Bakari (kushoto) akijadili jambo na Mtendaji Mkuu wa Umoja wa Mawasiliano Afrika Mashariki (EACO) Dkt. Yahya Simba wakati wa mapumziko ya staftahi, pembezoni mwa kikao-kazi cha Kamati-Tendaji ya Umoja huo kilichoketi Bububu, Zanzibar tarehe 28 Juni, 2022 kujadili usimamizi wa Mawasiliano baina na miongoni mwa nchi wanachama wa EAC. Picha: TCRA
Wakuu wa Taasisi za Usimamizi wa Mawasiliano Afrika Mashariki katika picha ya pamoja pembezoni mwa kikao-kazi cha Kamati-Tendaji ya Umoja wa Mawasiliano Afrika Mashariki (EACO-Exco); kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Masuala ya Utangazaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Sudani-Kusini, Elijah Alier Gai; Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Serikali wa Usimamizi wa Mawasiliano-Burundi, Samuel Muhizi; Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania -(TCRA) Dkt. Jabiri Bakari; Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano na Matumizi ya Mawasiliano-Rwanda Deo Muvunyi; Mkurugenzi Mkuu wa Kamisheni ya Mawasiliano-Uganda, Irene Kaggwa Sewankambo, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Kenya Ezra Chiloba na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Sudani Kusini, Napoleon Adok Gai. Picha na TCRA.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Dkt. Jabiri Bakari (wa pili kutoka kushoto) akiwasilisha hoja kwenye kikao-kazi cha Kamati-Tendaji ya Umoja wa Mawasiliano Afrika Mashariki (EACO) kilichofanyika Bububu, Zanzibar; wengine pichani ni Mtendaji Mkuu wa EACO Dkt. Ally Simba (wa kwanza-kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa Kamisheni ya Mawasiliano-Uganda, Irene Kaggwa Sewankambo (wa kwanza kulia), na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano-Kenya Ezra Chiloba. Kikao hicho cha kawaida cha kazi kiliweka mikakati ya uboreshaji usimamizi huduma za mawasiliano baina ya nchi wanachama. Picha na: TCRA
Wakuu wa Taasisi za Usimamizi wa Mawasiliano Afrika Mashariki (walioketi) na wataalam wa mawasiliano kutoka Mamlaka za Usimamizi wa mawasiliano Afrika Mashariki katika picha ya pamoja pembezoni mwa kikao-kazi cha Kamati-Tendaji ya Umoja wa Mawasiliano Afrika Mashariki (EACO-Exco); walioketi kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Masuala ya Utangazaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Sudani-Kusini, Elijah Alier Gai; Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Serikali wa Usimamizi wa Mawasiliano-Burundi, Samuel Muhizi; Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania -(TCRA) Dkt. Jabiri Bakari; Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano na Matumizi ya Mawasiliano-Rwanda Deo Muvunyi; Mkurugenzi Mkuu wa Kamisheni ya Mawasiliano-Uganda, Irene Kaggwa Sewankambo, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Kenya Ezra Chiloba na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Sudani Kusini, Napoleon Adok Gai. Mkutano huo ulijadili masuala ya usimamizi wa mawasiliano katika ukanda wa Afrika Mashariki. Picha na TCRA.
Wajumbe wa Kamati-Tendaji ya Umoja wa Mawasiliano Afrika Mashariki (EACO-ExCo) wakimsikiliza kwa makini Mtendaji Mkuu wa Umoja huo Dkt. Ally Yahya Simba anaesisitiza jambo wakati wa mapumziko mafupi pembezoni mwa kikao-kazi cha kamati hiyo kilichoketi Bububu, Zanzibar mapema wiki hii kujadili maendeleo ya usimamizi wa sekya ya mawasiliano. Wanaomsikiliza Dkt. Ally kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Dkt. Jabiri Bakari, Afisa Utawala na Rasilimali Watu-TCRA Erasmo Mbilinyi na Mwezeshaji kutoka Taasisi ya Uongozi Institute. Picha na TCRA
0 Comments