Mkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu Dkt. John Kalage akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 16,2022 Jijini Dar es Salaam wakati akitoa maoni kuhusu Bajeti iliyowasilishwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt Mwigulu Nchemba juzi Bungeni Jijini DodomaMkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu Dkt. John Kalage akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 16,2022 Jijini Dar es Salaam wakati akitoa maoni kuhusu Bajeti iliyowasilishwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt Mwigulu Nchemba juzi Bungeni Jijini Dodoma.Meneja Idara ya Utafiti, Ubunifu na Uchambuzi wa Sera-HakiElimu Bw.Mwemezi Makumba, akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 16,2022 katika Ofisi za HakiElimu Jijini Dar es Salaam
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
***************************
Na Magrethy Katengu, DAR ES SALAAM
Shirika lisilo la kiserikali linaloshughulikia masuala ya elimu nchini, Haki Elimu limefurahishwa na Serikali kwa uamuzi wa kufuta ada ya wanafunzi wanaojiunga na masomo kidato cha tano na sita ambapo inakwenda kusaidia baadhi ya wanafunzi wanaotokea katika familia zenye kipato cha chini.
Akizungumza na Waandishi wa habari leo Juni 16,2022 Jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Haki Elimu Dkt. John Kalage wakati akitoa maoni kuhusu Bajeti iliyowasilishwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt Mwigulu Nchemba juzi Bungeni Jijini Dodoma ambapo amesema Uamuzi huo unatarajia kuwanufaisha takribani wanafunzi wapatao 95,000 wa kidato cha tano na zaidi ya 60,000 wa kidato cha sita ambapo Serikali itaongeza zaidi ya billion 10.3 katika Bajeti ya utoaji elimu bila malipo
"Hii ni moja ya pendekezo Muhimu sana Haki elimu tunaunga mkono hivyo utoaji wa elimu bila malipo inasaidia sana hata wazazi wasio na uwezo wa kuwaendeleza watoto wao watakosa sababu hivyo haizuii kuchangia michango mingine midogomidogo".Amesema Dkt Kalage
Aidha amesema Bajeti ya Taifa Serikali kupitia Wizara ya Fedha na mipango imewasilisha TZS Trillion 41.48 kama mapendekezo na matumizi ya mwaka 2022/2023 huku sekta ya Elimu ikitengewa Bajeti ya 5.64 ikiongezeka kutoka 5.3 ya mwaka 2021/2022
"Kiwango kilichotengwa kwa ajili ya Sekta ya elimu ni sawa na asilimia 13.6 ya Bajeti pendekezwa ya Taifa Kwa mujibu wa mapendekezo ya kitaifa ,kikanda na kimataifa ni Muhimu bajeti ya elimu kuwa walau asilimia 20 ya Bajeti mfano Mpango wa tatu wa Maendeleo ya Elimu unapendekeza kuwa bajeti Kwa mwaka wa Fedha 2022 iwe Trion 7.39 kiwango ambacho kingekuwa ni sawa na asilimia 18 ya Bajeti ya mwaka wa Fedha 2022/2023"alisema Dkt Kalage
Hata hivyo Haki Elimu imeiomba Serikali kuhakikisha wanazingatia hali halisi ya mahitaji ya wanafunzi wa kidato cha tano na sita na ijiepushe kupeleka ruzuku katika kiwango na utaratibu unaotumika kwa madarasa ya chini kwani suala la ruzuku shuleni limezungumzwa na wadau wengi hazitoshi kuendesha shule zetu hivyo kiwango hiko cha 10,000 wa kila mwanafunzi wa shule ya msingi kiongezwe Hadi 25,000 na kutoka TZS 25,000 kwa mwanafunzi wa Sekondari hadi TZS 55,000 Kwa mwaka
0 Comments