Taasisi ya kifedha ya Faidika Microfinance Tanzania imetenga zaidi ya shillingi bilioni 20 kwa ajili ya kukopesha wafanyabiashara wadogo na wa kati kupitia program yao ijulikanayo kwa jina la “MKOPO FASTA”.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Faidika Microfinance Tanzania, Bw. Baraka Munisi amesema kuwa mkopo huo utolewa kwa muda mfupi na masharti nafuu na kuwaomba wafanyabishara wachangamikie kukopa.
Bw. Munisi alisema kuwa sababu ya Faidika Microfinance kutoa mkopo huo ni kuwainua vipato wafanyabishara ili kuwawezesha kupata maendeleo kama kauli mbiu yao ya ‘’Lets Improve Life’’ inavyosema.
Kwa mujibu wa Bw Munisi wanajua changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo wafanyabisahara hao na hivyo kuamua kuleta mpango huo maalum wa kuwasaidia kuzikabili changamoto hizo.
Alifafanua kuwa ili mfanyabiashara aweze kupata mkopo, anahitaji kuwa na leseni ya biashara, namba ya utambulisho wa mlipa kodi (TIN) na cheti kilichohidhinishwa cha ushuru, picha, kitambu-lisho cha serikali kinachotambulika.
“Miezi kadhaa iliyopita Faidika ilizindua programu ya “LetsGO Digital Mall” ambayo unamwezesha mteja wao kupata huduma bora kwa njia rahisi na haraka zaidi.
Kupitia LetsGo Digital Mall, mteja anaweza kujihudumia wenyewe kutoka kiganjani mwa simu yake. Tunaamini njia hii itarahisisha mteja kupata mkopo wa kibiashara kwa urahisi zaidi,” alisema Bw. Munisi.
Kwa upande wake, Mkuu wa kitengo cha Mauzo, Masoko na Mifumo wa Faidika Microfinance Tanzania, Bw. Asupya Bussi Nalingigwa alisema kuwa wamejipanga kutoa huduma bora zaidi kwa wateja wao na kuwaomba kuanza kuwasilisha maombi. Bw. Nalingigwa alisema kuwa taasisi yao inajivunia kutoa huduma bora za kifedha na jambo zuri zaidi ni kuwa na matawi mengi ya kutoa huduma hiyo hapa nchini.
“Ni fursa kwa wafanyabiashara wadogo wadogo na wakati kupata mkopo kutoka taasisi yetu, tena wenye mashari nafuu na kwa njia ya haraka zaidi.
Tunawakaribisha ili kuweza kuinua biashara zao na vilevile kipato,” hapa kwetu mambo yote ‘’MKOPO FASTA ‘’alisema Bw Nalingigwa.
Alifafanua kuwa ili kuweza kuwafikia wateja wengi taasisi yao imeanzisha namba maalum ambapo mteja anatakiwa kutuma neno FAIDIKA kwenda namba 15062 kisha kuchagua ‘’1’’ na kuanza kupata huduma kutoka kwa maofisa wao.p>
0 Comments