Ticker

6/recent/ticker-posts

BENKI YA NBC YAFUNGUA MILANGO ZAIDI KWA WAFANYABIASHARA WA TANZANIA NA AFRIKA KUSINI


Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Bw.Theobald Sabi akizungumza na wajumbe wa Jukwaa la Wafanyabiashara wa Afrika Kusini na Tanzania wakati wa Mkutano wa Jukwaa hilo ulifanyika jijini Dar es Salaam 


Mwenyekiti wa Jukwaa la Wafanyabiashara wa Afrika Kusini, Bw. Manish Thakrar (katikati) akizungumza na wajumbe wa jukwaa hilo wakati wa Mkutano wa Jukwaa hilo ulifanyika jijini Dar es Salaam


Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Bw. Theobald Sabi (Kushoto) akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wafanyabiashara wa Afrika Kusini, Bw. Manish Thakrar wakati wa Mkutano wa Jukwaa hilo ulifanyika jijini Dar es Salaam


Wajumbe wa Jukwaa la Wafanyabiashara wa Afrika Kusini na Tanzania wakifuatilia Mkutano wa Jukwaa hilo ulifanyika jijini Dar es Salaam jana.

..............................

Na Mwandishi Wetu-DAR ES SALAAM

BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imesisitiza kuhusu utayari wake katika kufanikisha ustawi wa biashara baina ya Tanzania na Afrika kusini kupitia huduma zake hususani kwa katika uwekezaji wa biashara na kilimo.

Msimamo huo wa benki hiyo umetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Bw Theobald Sabi wakati akizungumza kwenye Mkutano wa Jukwaa la Wafanyabiashara wa Afrika Kusini uliofanyika jijini Dar es Salaam jana.

Bw. Sabi alisema kwa muda mrefu sasa benki hiyo imekuwa mdau mkubwa wa wafanyabiashara kati ya Afrika Kusini na Tanzania ambapo kupitia mkutano huo aliweza kuelezea huduma mbalimbali zinazotolewa na benki hiyo kwa wafanyabiashara hao ikiwemo huduma za huduma za mikopo ya biashara na kilimo.

“Jukumu letu kama benki kubwa hapa nchini ni kuhakikisha tunatoa masuluhisho ya kibiashara kwa wafanyabiashara wetu ili waweze kufanya shughuli zao kiushindani ndani na nje ya nchi. Tumekuwa tukitoa huduma mbalimbali kwao ikiwemo mikopo ya aina mbalimbali ikiweo ya biashara na kilimo, bima kupitia benki sambmba na kuhusumia mnyororo wote wa biashara ikiwemo kuhifadhi fedha, kutuma na kupokea fedha kutoka ndani nan je ya nchini,’’ alisema.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jukwaa la Wafanyabiashara wa Afrika Kusini, Bw. Manish Thakrar alisema umuhimu wa benki ya NBC na taasisi nyingine za kifedha ni mkubwa hususani katika kipindi hiki ambacho kuna ongezeko kubwa la biashara baina ya Tanzania na Afrika Kusini.

“Tunawashukuru sana NBC tumekuwa nao kwa muda mrefu lakini kwasasa tunawahitaji zaidi. Changamoto ya COVID 19 pamoja na vita inayoendelea baina ya Urusi na Ukraine imeongeza sana mahitaji ya bidhaa hususani za vyakula nchini Afrika Kusini hivyo kwetu hiyo inaweza kuwa fursa kubwa ikiwa tutachangamkia. Hata hivyo habari njema ni kuwa benki ya NBC imeonyesha kutoa kipaumbele pia kwenye mikopo ya kilimo hilo litatusaidia sana kwa kuwa bidhaa za vyakula zinahitajika zaidi huko Afrika Kusini,’’ alisema.

Post a Comment

0 Comments