Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb), Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa ameongoza ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mkutano wa Kisekta wa Mawaziri wenye dhamana ya kusimamia Ulinzi, Amani na Usalama kutoka Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika uliofanyika jijini Addis Ababa, Ethiopia tarehe 12 Mei, 2022.
Mkutano huu ambao ni wa kwanza kufanyika ana kwa ana tangu mlipuko wa ugonjwa wa UVIKO-19 mwaka 2020, ulitanguliwa na Mkutano wa Wataalam ambao ulifanyika tarehe 09 na 10 Mei, 2022 na kufuatiwa na Mkutano wa Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi, Amani na Usalama ambacho uliofanyika tarehe 11 Mei, 2022.
Pamoja na mambo mengine, mkutano huo unafanyika kwa lengo la kujadili ushirikiano kati ya Umoja wa Afrika, Mashirika ya Kikanda na Nchi Wanachama kuhusu Majeshi ya Akiba ya Afrika. Pia, mkutano utapitia na kupitisha Sera mbili kuhusu umuhimu wa kutoa kipaumbele kwa ulinzi wa watoto na haki zao wakati wa Operesheni za Kulinda Amani barani Afrika (Child Protection in African Union Peace Support Operations (2021) and Mainstreaming Child Protection in the African Peace and Security Architecture).
Kadhalika, mkutano huo ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika kuhusu Ugaidi na Mabadiliko ya Serikali kinyume cha Katiba ambao umepangwa kufanyika Malabo, Guinea ya Ikweta tarehe 28 Mei, 2022.
Ujumbe wa Mhe. Waziri Tax unamjumuisha pia Mhe. Hamad Masauni (Mb), Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Nyakoro Sirro na Maafisa wengine Waandamizi wa Serikali.
Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb), Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa ameongoza ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mkutano wa Kisekta wa Mawaziri wenye dhamana ya kusimamia Ulinzi, Amani na Usalama kutoka Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika uliofanyika jijini Addis Ababa, Ethiopia tarehe 12 Mei, 2022. Pichani ni Wajumbe walioshiriki Mkutano huo akiwemo Dkt.Tax
0 Comments