Ticker

6/recent/ticker-posts

WAZIRI UMMY :TUTASHIRIKIANA NA WADAU KUWA NA ENEO LA WATOTO KUSHEHEREKEA SIKUKUU JIJINI TANGA

WAZIRI wa Afya na Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu akizungumza jambo mara baada ya kutoka Msikiti wa Ijumaa kulipofanyika swala ya Eid El Fitri Kimkoa

WAZIRI wa Afya na Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu akitoa kwenye msikiti mkuu wa Ijumaa Jijini Tanga mara baada ya swala ya Eid El Fitri
WAUMINI wa dini ya Kiislamu Jijini Tanga wakiswali swala ya Eid El Fitri katika Msikiti Ijumaa Jijini Tanga leo
WAZIRI wa Afya na Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu katika akiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kumalizika swala ya Eid El Fitri
WAZIRI wa Afya na Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu katika akiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kumalizika swala ya Eid El FitriWAZIRI wa Afya na Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu katika akiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kumalizika swala ya Eid El Fitri

WAZIRI wa Afya na Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu kushoto akiwa na nje ya msikiti wa Ijumaa mara baada ya kumalizika swala ya Eid El Fitri leo

NA MWANDISHI WETU,TANGA.

WAZIRI wa Afya na Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu leo ameshiriki katika swala ya Eid El Fitri kwenye Msikiti wa Ijumaa Jijini humo huku akihaidi kushirikiana na wadau kuhakikisha wanakuwa na eneo la watoto kusheherekea sikukuu.

Ummy aliyasema hayo mara baada ya kumalizika kwa swala hiyo iliyohudhuriwa na waumini kutoka maeneo mbalimbali Jijini humo ambapo alisema kwamba wanafahamu Jiji hilo bado halina sehemu kuchezea watoto hivyo atalifanyia kazi.

Alisema kwamba eneo hilo ambalo wanatarajia kuhakikisha linakuwepo kwenye Jiji hilo litawezesha wazazi kwenda kusheherekea na watoto sikukuu na hilo atakwenda kuona namna ya kulifanyia kazi.

“Tunafahamu Jiji la Tanga bado halina sehemu ya kuchezea watoto kwa hiyo tutalifanyia kazi kwa kushirikiana na wadau kuhakikisha kuna kuwa na eneo kubwa na nzuri ambayo mzazi atakwenda kusheherehea na watoto sikukuu”Alisema

“Lakini pia katika sikukuu hii niwatakie kilalaheri wananchi wa Jimbo la Tanga na niwashukuru kwa heshima kubwa ambayo mmeendelea kunipa tutaendelea kushirikiana”Alisema

Aidha pia Waziri Ummy aliwataka wakazi wa Tanga mjini heri ya sikuuu ya Eid El Fitri huku akimuomba Mwenyezi Mungu azikubali funga zao na azipokee dua zilizofanyika kipindi cha mwezi wa ramadhani.

Waziri huyo aliwataka wananchi kuendelea kutenda mema kupendana na kushirikiana na kufanya ibada ya kujinyenyekeza kwa mungu na wasichoke kumuomba mwenyezi mungu.

Hata hivyo aliwataka watoto washeherekee vizuri sikukuu isifike usiku huku akiwataka wanapotoka kwenda kutembea watoto waende na watu wazima ambao watawasimamia kwa sababu kwenye kipindi cha idd kuna watu wanaweza kufanya mambo maovu. Mwisho.

Post a Comment

0 Comments