***************
Na.WAF-Dodoma
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu leo amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye kikao cha pili cha 'Global Covid-19' kwa njia ya mtandao ulioandaliwa za Serikali ya Belize, Ujerumani, Indoneaia, Senegal na Marekani.
Katika kikao hicho Waziri Ummy amesema hadi kufikia tarehe 9 Mei, 2022 jumla ya dozi 7,713,526 za chanjo ya UVIKO-19 zimetolewa nchi nzima na watu wapatao 4,110,884 sawa na asilimia 13.37 wamepata chanjo hiyo ambayo makadirio yake ni kuchanja watanzania wapatao 30,740,928.
Waziri Ummy amesema hadi sasa Tanzania imeshapokea dozi 11,232,374 kutoka COVAX facility pamoja na washirika wengine.
Vilevile Waziri Ummy ameeleza katika kikao hicho kuwa Serikali ya Tanzania itaendelea kuchukua hatua mbalimbali kuhakikisha wananchi wanapata Chanjo dhidi ya UVIKO-19 ikiwemo kutoa elimu ya umuhimu wa chanjo kwa kuwa hatujui wimbi jingine la Kirusi litakuaje.
0 Comments