Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mhe. Innocent Bashungwa akizungumza na waandishi wa habari wakati akitangaza Matokeo ya uchaguzi wa wanafunzi kujiunga na kidato cha tano, vyuo vya ualimu na vyuo vya elimu za ufundi, Leo Mei 12, 2022 Dar es salaam. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mhe. Innocent Bashungwa akitangaza Matokeo ya uchaguzi wa wanafunzi kujiunga na kidato cha tano, vyuo vya ualimu na vyuo vya elimu za ufundi, Leo Mei 12, 2022 Dar es salaam. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mhe. Innocent Bashungwa akitangaza Matokeo ya uchaguzi wa wanafunzi kujiunga na kidato cha tano, vyuo vya ualimu na vyuo vya elimu za ufundi, Leo Mei 12, 2022 Dar es salaam.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
***********************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
WANAFUNZI 153,219 wakiwemo wasichana 67,541 na wavulana 85,678 sawa na asilimia 91.8 ya wenye sifa wamechaguliwa kujiunga na shule za Sekondari Kidato cha Tano, Vyuo vya Ualimu na Vyuo vya Elimu ya Ufundi mwaka 2022.
Wanafunzi 90,825 wakiwemo wasichana 43,104 wamechaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano katika Shule mpya 22 za Serikali zilizoanza mwaka 2022.
Ameyasema hayo leo Mei 12, 2022 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mhe. Innocent Bashungwa wakati akitangaza Matokeo ya uchaguzi wa wanafunzi kujiunga na kidato cha tano, vyuo vya ualimu na vyuo vya elimu za ufundi Jijini Dar es salaam.
Amesema kati ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano, wapo wanafunzi wenye mahitaji maalum 481, ambao kati yao wasichana ni 204.
"Kati ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano, wanafunzi 41,401 wakiwemo wasichana 17,390 watajiunga kusoma tahasusi za Sayansi na Hisabati na wanafunzi 49,133 wakiwemo wasichana 25,508 watajiunga kusoma tahasusi za masomo ya Sanaa,Lugha na Biashara". Amesema Waziri Bashungwa.
Aidha Waziri Bashungwa amesema kwa kuangalia takwimu za mwaka 2022, kumekuwa na ongezeko la wasichana 7,555 waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi, ukilinganisha na mwaka 2021 hata hivyo idadi hii bado ni ndogo kulinganisha na wavulana.
"Ili kukabiliana na changamoto hii, Wizara inaendelea kuboresha miundombinu ya shule ili kuhakikisha wasichana wengi zaidi wanajiunga na Kidato cha Tano". Amesema Waziri Bashungwa.
Pamoja na hayo Waziri Bashungwa amesema jumla ya wanafunzi 14,254 wakiwemo wasichana 3,901 na wavulana 10,353 wamekosa nafasi ya kujiunga na Kidato cha tano na Vyuo vya Ualimu na Vyuo vya Elimu ya Ufundi mwaka 2022.
0 Comments