******************************
Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mindi Kasiga ametoa wito kwa wadau wa Utalii kutumia ubunifu zaidi katika kutangaza vivutio vya utalii wa ndani ili kukuza sekta ya utalii na kuongezea pato la taifa.
Ameyasema hayo katika maonyesho jijini Dar es salaam kuelekea wiki ya Ubunifu yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu ,Sayansi na Teknelojia kwa kushirikiana na Tume ya Taifa ya Sayansi ya Teknolojia(COSTECH) pamoja na UNDP kupitia Programu yake ya Funguo
Amesema kuwa Wizara itahakikisha inatoa ushirikiano kwa wabunifu waliopo nchini katika kuwawezesha kutangaza bunifu zao ndani na je ya Tanzania.
"Kuna mambo yanayojitokeza katika mazingira ya sasa kwenye sekta ya utalii ambayo ni muhimu sana kuhusisha ubunifu wa teknolojia katika kutangaza vivutio vya utalii,” Amesema Balozi Mindi
Naye Mkurugenzi wa Kodi kutoka kampuni ya KPMG Donald Nsanyikwa amesema kuwa Kwa wabunifu Moja ya jambo la msingi wanalopaswa kuzingatia ni masuala ya kodi.
“Tumejaribu kuwalezea wabunifu wakiwemo wanaojihusisha na ujasiriamali kuwa wanapoona watu wa TRA wanakuja kwenye biashara zao wasione kama wanawaingilia bali jukumu lao kubwa ni kuwapa elimu ya kujua umuhimu wa kodi pindi wanapoanza biashara,” Amesema Mkurugenzi Donald.
0 Comments