Mkurugenzi wa utafiti,sera na Mipango kutoka Mamlaka masoko mitaji na dhamana Alfred Mkombo akizungumza na waandishi wa habari katika Warsha ya ubunifu na utafiti.
Promisi Mwakale kutoka tume ya Sayansi na teknolojia COSTEC
Pol Damota Mtaalamu wa fedha Mfuko wa mtaji wa maendeleo kutoka Umoja wa mataifa UNCDF
Daniela kwayu Mkurugenzi wa kampuni ya iliyojikita katika kilimo na teknolojia Farm Agri akizungumza na waandishi wa habari.
***********
Na Magrethy Katengu
Vijana wa kitanzania wamewatakiwa kuchangamkia fursa ya bunifu za kibiashara ili kusaidia Taifa kufikia azma ya serikali ya mapinduzi ya nne ya viwanda kuelekea maendeleo endelevu Duniani.
Rai hiyo imetolewa leo Jijini Dar es salaam na Mkurugenzi wa utafiti,sera na Mipango kutoka Mamlaka masoko mitaji na dhamana Alfred Mkombo katika Warsha ya ubunifu na utafiti iliyofanyika lengo likiwa kuangalia namna ya kusaidia biashara ndogo za Kati na kubwa Kwa kuziwezesha kupata fedha il kukuza ama Kwa kuuza hisa au vipande vya Uwekezaji vya pamoja au hatii fungani ili kukuza mimitaji yao kupitia bunifu zinazofanywa.
"Ili uweze kuendeleza masoko na mitaji lazima usimamie biashara bunifu ,bidhaa na huduma zinazohitajika kwa wananchi hivyo tunawaasa vijana muwe wabunifu zaidi na zaidi kwani tumekuwa tukifanya Mipango mbalimbali ili kuwasaidia Kwa kukusanya fedha kupitia mitandao,majukwaa na tunaandaa miongozo na sera Sasa mkiendelea kukaa na kusema hakuna ajira kazi kwenu"alisema Alfredi.
Kwa upande wake Daniela kwayu Mkurugenzi wa kampuni ya iliyojikita katika kilimo na teknolojia Farm Agri ambapo wao wamekuwa waniwasaidia wakulima kupata fedha za kuendesha shughuli zao Kwa kupata pembejeo na kuendesha miradi yao kwa kulima kilimo bora na kupata malighafi zenye ushindani wa masoko.
"Uchumi hauwezi kukua kama hauwezi kuwekeza kwenye kilimo kwani kilimo ni uti wa mgongo Kwa watu wali wengi wanahitaji fedha ili wazalishe Kwa wingi na wajikomboe na umasikini "alisema Daniela.
Promisi Mwakale kutoka tume ya Sayansi na teknolojia COSTEC wamekuwa wakitoa wakifungua masoko Kwa ajili ya wabunifu wenye mawazo Kwa kutoa ruzuku Kwa ajili ya kuwasaidia wabunifu bila kuangalia jinsia kwani watoto wa kike kwa kutumia njia mbalimbali kuwaendeleza katika teknolojia nao wanapatiwa ruzuku.
Nae Pol Damota Mtaalamu wa fedha Mfuko wa mtaji wa maendeleo kutoka Umoja wa mataifa UNCDF ni miongoni mwa wadhamini wa wiki ya ubunifu wamekuwa wakisaidia sera katika idara mbalimbali za serikali katika kutengeneza mazingira wezeshi Kwa wabunifu kuweza kujaribu ubunifu wao Kwa muda ili waweze kupata leseni
Tumekuwa na mifumo Kwa wabunifu walioendelea zaidi Kwa kuwapatia mikopo na elimu ili kukuza biashara zao Kwa kutumia teknolojia iliyopo ili waweze kukua na kuongezeka mijini vijijini zaidi"alisema Damota
Aidha wiiki ya maonyesho ya Ubunifu inaratibiwa na Wizara ya Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na COSTECH na UNDP kupitia program yake ya Ubunifu-Funguo. Mdhamini mkuu ni Vodacom Tanzania.kilele Cha wiki hiyo inatarajiwa kufanyiwa Dodoma mei 16-20, 2022 Watu wote wanakaribishwa.
0 Comments