Ticker

6/recent/ticker-posts

TAASISI YA DR. REGINALD MENGI (DRMF) IMEKUTANISHA WATU WENYE ULEMAVU KATIKA KUMBUKIZI YA MUASISI WAO DR. REGINALD MENGI.


*************************

Halfa hiyo iliyofanyika Jana katika viwanja vya 'Jakaya Kikwete Youth Park' ilifunguliwa rasmi na Mheshimiwa Profesa Joyce Ndalichako, Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira, Vijana, na Wenye Ulemavu) aliyewakilishwa na Mkurugenzi wa Kuongeza Tija katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Yohana Medadi.

Halfa hii pia ilihudhuriwa na wageni mbalimbali akiwemo Balozi wa Marekani nchini Tanzania Mh. Dkt. Donald Wright, Balozi wa Kanada nchini Tanzania Mh. Pamela O’Donell, Balozi wa heshima wa Shelisheli nchini Tanzania, Bi. Maryvoone Poole na Mkurugenzi wa Elimu Jumuishi na Maalum Dkt. Magreth Matonya.

Pamoja nao walikuwemo wakuu mbalimbali wa mashirika binafsi na viongozi wa taasisi zisizo za kiserikali

Hafla hii ilikuwa maalumu kwaajili ya kukumbuka na kusheherekea maisha ya Dr. Reginald Mengi na moyo wake wa kizalendo wa kujitolea kwa jamii hapa nchini Tanzania. Wakati wa uhai wake alijitoa kikamilifu kuwasaidia watu wenye ulemavu katiks njanja mbalimbali ikiwemo elimu afya pamoja na kutetea haki za watu wenye ulemavu hususani kukemea vitendo vya kukatili dhidi yao.

Kwa kipindi cha miongo mitatu alikuwa akiwakutanisha watu wenye ulemavu zaidi ya 5000 kila mwaka na kula nao chakula cha mchana. Hii ilikuwa nafasi ya kuielimisha jamii kuwa watu wenye ulemavu wana haki sawa na wanatakiwa kupendwa na kulinda utu wao.

Akizungumzia hafla hiyo Mkurugenzi wa Taasisi ya Dk Mengi Foundation(DRMF) Bi. Shimimana Ntuyabaliwe mbali na pongezi na salamu zake za shukrani kwa Serikali kwa ushirikiano ambao wamekuwa wakiupata, vilevile aliwashukuru watu wenye ulemavu kwa kuwapa ushirikiano na kuendelea kuwaamini katika harakati za kutetea ustawi wa wa mtu mwenye ulemavu.

Vilevile aliwashukuru wageni na washiriki wote kwa kushiriki hafla hiyo. Alisema tukio hilo ni faraja kwa taasisi hiyo kutokana na kuenzi kwake mchango wa Dk Mengi. Akimalizia hotuba yake alisema kuwa tarehe 29 Mei ambayo ni siku ya kuzaliwa kwa Dr. Mengi itakuwa ndio siku maalum ya kumbukizi yake na kuwa wataifanya kila mwaka kumuenzi na kusheherekea maisha yake.

Naye mjane wa Dr. Reginald Mengi, Bi Jacqueline Mengi alisema kuwa ingawa wao kama familia wana huzuni ya kuondokewa na mume na baba wa familia, lakini wanapata faraja kubwa kwa kuwa na ndugu wanaowafariji hususan watu wenye ulemavu. Vilevile aliahidi kutumia uwezo wake kuendeleza ndoto za mume wake katika taasisi hii.

Mbali na matukio ya upimaji wa afya, tezi dume na kupata miwani bure pia washiriki wa hafla hiyo akiwemo Mgeni rasmi, Bw. Yohana Madadi, mke wa Dk Mengi, Jacqueline Mengi na Mh. Pamela O’Donnell walishiriki michezo jumuishi ikiwa ni pamoja na Amputee Football na Wheel chair basketball. Michezo mbalimbali jumuishi ilisherehesha na kupamba siku hii ikiwa ni pamoja na mpira wa pete kwa viziwi unaoendeshwa kwa kutumia lugha ya alama, mpira wa kengele (goal ball) kwa watu wasioona na mchezo maalum uliochezwa na timu ya Tembo Warriors ambao wafuzu kuwania kombe la dunia la Amputee Football baadae mwaka huu nchini Uturuki

Sherehe hii ya kumbukizi ilihudhuriwa na watu wenye ulemavu wapatao 1,000 ambao walishiriki michezo upimaji afya pamoja na chakula cha mchana pamoja na wageni.

DRMF pia ilikabidhi jezi za michezo pamoja na mipira wa miguu kwa wasichana ya Jakaya Kikwete Youth Park, Mashuka kwa Shule za Jeshi la Wokovu pamoja na Mtoni Viziwi.

Post a Comment

0 Comments