Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda akimsikiliza Mkuu wa kiwanda cha kuchapiaha vitabu cha PRESS B Bw.Adonia Mpemba mara baada ya kufanya ziara ya kutembelea Press A Magogoni na Press B leo Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda akiangalia namna uchapishaji wa vitabu vya uono hafifu ukifanyika mara baada ya kufanya ziara ya kutembelea Press A Magogoni na Press B leo Jijini Dar es SalaamWaziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda akitazama baadhi ya vitabu vilivyochapishwa katika kiwanda cha Press A mara baada ya kufanya ziara ya kutembelea Press A Magogoni na Press B leo Jijini Dar es SalaamWaziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda akitazama moja ya kitabu kilichochapwa katika kitui cha Press A Magogoni mara baada ya kufanya ziara ya kutembelea kituo hicho na Press B leo Jijini Dar es SalaamWaziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda akimsikiliza Mkuu wa kiwanda cha PRESS A Bw.John Kaswalala Jijini Dar es Salaam mara baada ya kufanya ziara ya kutembelea Press A Magogoni na Press B leo Jijini Dar es SalaamWaziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kufanya ziara ya kutembelea Press A Magogoni na Press B leo Jijini Dar es SalaamWaziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda akisalimiana na baadhi ya watumishi wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) mara baada ya kufanya ziara ya kutembelea Press A Magogoni na Press B leo Jijini Dar es Salaam.
*******************
SERIKALI inatumia shilingi Bilioni 15 kila mwaka kuchapisha vitabu vya nukta nundu vinavyotumiwa na wanafunzi wasioona na wenye uoni hafifu.
Hiyo inatokana na malighafi ya karatasi inayotumika kuchapa inanunuliwa Dubai na Marekani.
Ameyasema hayo leo Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda wakati akifanya ziara ya kutembelea vituo vya kuchapisha vitabu ambapo ametembelea kituo cha Press A Magogoni na Press B kilichopo shule ya Uhuru Mchanganyiko Jijini Dar es Salaam.
Aidha Prof.Mkenda ameitaka Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) kuweka mkakati ndani ya mwaka mmoja iwe imepata mashine kubwa ya kuchapa na kutafuta tenda nafuu ya malighafi ya karatasi.
"Dubai ni Jangwani, hakuna miti wakati hawazalishi karatasi, sisi tunaenda kuchapa huko kwa fedha nyingi, nataka na sisi tukanunue malighafi huko wanakonunua wao tuchapishe wenyewe."Amesema Prof.Mkenda.
"Wafadhili wanaotupatia fedha masharti tenda ya kuchapa itangazwe kimataifa, sasa badala sisi tutangaze tenda ya kuchapiwa bora tutangaze tenda ya kupata mashine kubwa ya kisasa hii itapunguza gharama." Amesisitiza
Amesema mashine kubwa zaidi ya uchapaji huuzwa shilingi bilioni 30, hivyo watazungumza na wafadhili kuwaeleza wafanikishe hilo, kwani wanatekeleza manunuzi ya kimataifa ikiwa ni moja ya sharti la wafadhili hao.
Amesema serikali imedhamiria kuimarisha uchapishaji kwa kuiwezesha TET kupata karatasi kwa bei nafuu, umeme wa uhakika na mashine kubwa ya kisasa ya uchapaji.
Kupitia fedha za Covid 19 zilizotolewa na Rais Samia Suluhu imewezesha TET kuchapa vitabu vya nukta nundu vyote vya kidato cha kwanza hadi cha sita.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa TET Dkt. Aneth Kombat akizungumza awake amesema sababu ya kutochapa nchini ni gharama kubwa ya karatasi, kutokuwepo kwa umeme wa uhakika na wa bei nafuu na mitambo ya kutosha kumudu uchapaji kulingana na mahitaji
Amesema Kiwanda cha uchapaji cha Press A Magogoni ni moja kati ya viwanda saba vya taasisi hiyo na walikabidhiwa na wizara tangu mwaka 2019.
"Kiwanda hiki kinatumika kuchapa muongozo wa walimu darasa la awali hadi la saba na kwa mwaka huchapa vitabu milioni tatu ukihusisha na vya wenye uoni hafifu."Amesema
Pamoja na hayo amesema mahitaji ya vitabu hivyo yanakidhi ambapo wenye uoni hafifu wastani wa vitabu vitatu kwa mwanafunzi mmoja
0 Comments